Posted By Posted On

YANGA YAKOMAA NA MORRISON ALIYESAINI SIMBA, on September 4, 2020 at 9:00 pm

 UONGOZI  wa Klabu ya Yanga umekanusha vikali taarifa zinazoenea kwamba wameliondoa jina la winga, Benard Morrison kwenye orodha ya wachezaji wao katika usajili uliokamilika hivi karibuni. Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Saimon Patrick amesema timu yao ilipeleka jina la Bernard Morrison kwenye listi ya wachezaji wao wa 2020/21 lakini wameshangaa kuona Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) limeondoa jina hilo na kumuacha kwenye listi ya wachezaji wa Simba. Wakili huyo amesema wao kama Yanga walipeleka jina la Morrison ila wenye mamlaka ambao ni TFF ambao wao wameidhinisha acheze Simba lakini wao wamelipeleka mbele kusaka haki na kesi imeshafika Shirikisho la soka duniani (Fifa) kwa hiyo wana Yanga wasubiri haki yao. Yanga bado ipo kwenye mvutano na mchezaji huyo ambapo kesi ya mkataba wake ilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo TFF na mwisho wa siku Morrison alitangazwa kuwa mshindi.Ilianza kuskilizwa Agosti 10 mpaka Agosti 12 ambapo ilivuta hisia za mashabiki wengi na wadau wa michezo. Kwa sasa ameshaanza kutumika ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21.Amecheza mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii, Agosti 30 mbele ya Namungo FC wakati Simba ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku yeye akifunga bao moja na kusababisha penalti iliyofungwa na John Bocco.Alisaini dili la miaka miwili ndani ya Klabu ya Simba Agosti 8 akitokea Klabu ya Yanga ambayo bado inamtambua kwamba ni mchezaji wao halali.,


 UONGOZI  wa Klabu ya Yanga umekanusha vikali taarifa zinazoenea kwamba wameliondoa jina la winga, Benard Morrison kwenye orodha ya wachezaji wao katika usajili uliokamilika hivi karibuni.

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Saimon Patrick amesema timu yao ilipeleka jina la Bernard Morrison kwenye listi ya wachezaji wao wa 2020/21 lakini wameshangaa kuona Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) limeondoa jina hilo na kumuacha kwenye listi ya wachezaji wa Simba.

 

Wakili huyo amesema wao kama Yanga walipeleka jina la Morrison ila wenye mamlaka ambao ni TFF ambao wao wameidhinisha acheze Simba lakini wao wamelipeleka mbele kusaka haki na kesi imeshafika Shirikisho la soka duniani (Fifa) kwa hiyo wana Yanga wasubiri haki yao.

 

Yanga bado ipo kwenye mvutano na mchezaji huyo ambapo kesi ya mkataba wake ilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo TFF na mwisho wa siku Morrison alitangazwa kuwa mshindi.


Ilianza kuskilizwa Agosti 10 mpaka Agosti 12 ambapo ilivuta hisia za mashabiki wengi na wadau wa michezo. Kwa sasa ameshaanza kutumika ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21.


Amecheza mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii, Agosti 30 mbele ya Namungo FC wakati Simba ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku yeye akifunga bao moja na kusababisha penalti iliyofungwa na John Bocco.


Alisaini dili la miaka miwili ndani ya Klabu ya Simba Agosti 8 akitokea Klabu ya Yanga ambayo bado inamtambua kwamba ni mchezaji wao halali.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *