Posted By Posted On

Kessy: Sina muda mrefu Mtibwa,, on September 5, 2020 at 8:50 am

NA ZAINAB IDDY BEKI wa timu ya Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhan ‘Kessy’ amesema hatachezwa kwa muda mrefu katika kikosi hicho. Kessy amerejea katika kikosi cha Mtibwa Sugar, akiwa mchezaji huru, baada ya kumaliza kuitumikia Nkana FC ya Zambia. Akuzungumza na BINGWA jana, Kessy aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga, alisema malengo yake ni kucheza msimu mmoja,

NA ZAINAB IDDY

BEKI wa timu ya Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhan ‘Kessy’ amesema hatachezwa kwa muda mrefu katika kikosi hicho.

Kessy amerejea katika kikosi cha Mtibwa Sugar, akiwa mchezaji huru, baada ya kumaliza kuitumikia Nkana FC ya Zambia.

Akuzungumza na BINGWA jana, Kessy aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga, alisema malengo yake ni kucheza msimu mmoja wa Ligi Kuu Bara, kabla ya kwenda kusakata kabumbu nje ya Tanzania.

Kessy alisema amerejea nyumbani kwa lengo la kujipanga upya ili aweze kuendelea na harakati zake za kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu kubwa Afrika.

“Nilishuka kiwango na baada ya kugundua hilo nikaona sio vibaya kurudi nilikotoka nikajipange upya na ndicho kilichotokea nimerejea Mtibwa Sugar walikonilea.

“Mipango yangu ni kucheza msimu mmoja waligi ya nyumbani  ninaimani muda huo unanitosha kurejea kwenye kiwnago cha awali kisha mipango ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kuanza kufanyika  tena,” alisema Kessy

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *