Posted By Posted On

Larry Bwalya atoa ahadi tamu Simba,, on September 5, 2020 at 8:43 am

NA WINFRIDA MTOI KIUNGO mshambuliaji mpya wa Simba, Mzambia Larry Bwalya, ameahidi kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo, akipata nafasi ya kucheza dhidi ya Ihefu. Simba wanatarajiwa kucheza na Ihefu kesho ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Bwalya amejiunga na Simba katika kipindi,

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Simba, Mzambia Larry Bwalya, ameahidi kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo, akipata nafasi ya kucheza dhidi ya Ihefu.

Simba wanatarajiwa kucheza na Ihefu kesho ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Bwalya amejiunga na Simba katika kipindi cha dirisha kubwa la usajili la msimu huu akitokea Klabu ya Power Dynamol ya Zambia.

Tayari  kiungo huyo mshambuliaji ameanza kuonesha makali yake katika michezo ya kirafiki aliyocheza.

Akizungumza jana kupitia mtandao wa Klabu ya Simba, Bwalya, alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu ana deni kwa wapenzi wa timu hiyo.

Bwalya alisema atapambana kuhakikisha analipa deni na mashabiki wa Simba walionesha kumwamini.

 “Kila ninapoingia uwanjani najiona nina deni kwa sababu Wanasimba wana imani kubwa na mimi na sitaweza kuwaangusha nitahakikisha najituma ili kuwafurahisha,”alisema Bwalya.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *