Posted By Posted On

Simba wapata bosi mpya,, on September 5, 2020 at 8:56 am

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Klabu ya Simba, umemtangaza Hamis Kisiwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uanachama na mashabiki wa klabu hiyo. Kisiwa ambaye alikuwa meneja wa mashindano wa Simba, kwa sasa atashika nafasi hiyo baada ya  Hashimu Mbaga kutimuliwa mwezi uliopita. Kwa mujibu wa taraifa iliyotolewa na Simba jana na kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa,

NA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa Klabu ya Simba, umemtangaza Hamis Kisiwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uanachama na mashabiki wa klabu hiyo.

Kisiwa ambaye alikuwa meneja wa mashindano wa Simba, kwa sasa atashika nafasi hiyo baada ya  Hashimu Mbaga kutimuliwa mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa taraifa iliyotolewa na Simba jana na kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo,Mwina Kaduguda, Kisiwa ameanza majukumu mapya jana.

“Kuanzia sasa wanachama na mashabiki wote wa Simba wanapaswa kuwasiliana na Kisiwa katika masuala mbalimbali ya klabu.

“Kama wanachama na mashabiki wanahitaji ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu klabu au msaada wa jambo lolote lile mtu sahihi wa kumuona ni Kisiwa na sio mwingine kuanzia leo Septemba 4, hadi pale tutakapotoa taarifa ya mabadiliko kama ikibidi kufanya hivyo,” alisema Kaduguda.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *