Posted By Posted On

KLOPP HANA PRESHA NA USAJILI ,KUFYEKA NYOTA 10, on September 6, 2020 at 9:30 am

 JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa bado ana muda wa kufanya usajili hivyo kwa sasa hana presha.Liverpool ni mabingwa watetezi wa  Ligi Kuu England wanatarajiwa kuanza kwa kasi kutetea  taji hilo ambapo Septemba 12 wataanza kumenyana na Leeds wakiwa Anfield. Ripoti zinaeleza kuwa Klopp atafyeka majembe 10 ndani ya kikosi chake ili kupata nyota wengine wapya.Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye rada za Liverpool ni pamoja na Thiago Alacantra anayekipiga ndani ya FC Bayern Munich, raia wa Hisapnia.Kiungo huyo pia yupo kwenye rada za Manchester United ambao nao pia wanahitaji saini ya nyota huyo ambaye hivi karibuni alisema kuwa anafurahia maisha ndani ya Bayern Munich. Klopp amesema:”Sijui kitatokea nini kwa sasa ila bado tuna muda mpaka Oktoba 5 tutafanya mambo yetu kama ambavyo tumekuwa tukifanya.”,

 JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa bado ana muda wa kufanya usajili hivyo kwa sasa hana presha.


Liverpool ni mabingwa watetezi wa  Ligi Kuu England wanatarajiwa kuanza kwa kasi kutetea  taji hilo ambapo Septemba 12 wataanza kumenyana na Leeds wakiwa Anfield. 


Ripoti zinaeleza kuwa Klopp atafyeka majembe 10 ndani ya kikosi chake ili kupata nyota wengine wapya.


Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye rada za Liverpool ni pamoja na Thiago Alacantra anayekipiga ndani ya FC Bayern Munich, raia wa Hisapnia.


Kiungo huyo pia yupo kwenye rada za Manchester United ambao nao pia wanahitaji saini ya nyota huyo ambaye hivi karibuni alisema kuwa anafurahia maisha ndani ya Bayern Munich. 


Klopp amesema:”Sijui kitatokea nini kwa sasa ila bado tuna muda mpaka Oktoba 5 tutafanya mambo yetu kama ambavyo tumekuwa tukifanya.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *