Posted By Posted On

KMC KAMILI GADO KWA AJILI YA KUIVAA MBEYA CITY KESHO, on September 6, 2020 at 11:04 am

 UONGOZI wa KMC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Uhuru. Kikosi hicho  kinachonolewa na mzawa, Habibu Kondo kimefanya maandalizi yake ya mwisho leo Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwa timu hizi ndani ya msimu wa 2020/21.Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala imeeleza kuwa maandalizi ya kikosi yamekamilika kwa asilimia 100.”Hadi Sasa kikosi kimefanya maandalizi kwa asilimia 100 kipo tayari kwa ajili ya ushindani na kupata pointi tatu kwenye mchezo wetu dhidi ya Mbeya City. “Wachezaji wamejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho na mpaka sasa hakuna majeruhi ambaye yupo ndani ya timu hivyo imani ni kubwa kwa kikosi chetu kuweza kusaka pointi tatu kwenue mchezo wetu wa kesho ambao ni muhimu kwetu,” amesema.,


 

UONGOZI wa KMC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Uhuru. 


Kikosi hicho  kinachonolewa na mzawa, Habibu Kondo kimefanya maandalizi yake ya mwisho leo Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwa timu hizi ndani ya msimu wa 2020/21.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala imeeleza kuwa maandalizi ya kikosi yamekamilika kwa asilimia 100.

“Hadi Sasa kikosi kimefanya maandalizi kwa asilimia 100 kipo tayari kwa ajili ya ushindani na kupata pointi tatu kwenye mchezo wetu dhidi ya Mbeya City.

 “Wachezaji wamejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho na mpaka sasa hakuna majeruhi ambaye yupo ndani ya timu hivyo imani ni kubwa kwa kikosi chetu kuweza kusaka pointi tatu kwenue mchezo wetu wa kesho ambao ni muhimu kwetu,” amesema.,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *