Posted By Posted On

KUMEKUCHAAA, on September 6, 2020 at 11:53 am

NA WINFRIDA MTOI KIPYENGA cha Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21 kinatarajia kupulizwa leo kwa michezo sita kupigwa kwenye viwanja tofauti. Katika mtanange huo, wakongwe wa Kariakoo, bingwa mtetezi Simba atakuwa jijini Mbeya akichuana na wageni katika michuano hiyo, Ihefu FC saa 10:00 jioni Uwanja wa Sokoine. Yanga itakuwa jijini Dar es Salaam ikivaana
The post KUMEKUCHAAA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

KIPYENGA cha Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21 kinatarajia kupulizwa leo kwa michezo sita kupigwa kwenye viwanja tofauti.

Katika mtanange huo, wakongwe wa Kariakoo, bingwa mtetezi Simba atakuwa jijini Mbeya akichuana na wageni katika michuano hiyo, Ihefu FC saa 10:00 jioni Uwanja wa Sokoine.

Yanga itakuwa jijini Dar es Salaam ikivaana na Tanzania Prisons saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa, michezo hiyo inatarajia kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini.

Usajili wa wachezaji wenye majina makubwa ulifaonywa na klabu hizi msimu huu, ndiyo unaoshawishi mashabiki wao kutamani kuyapima mejembe yao, licha ya kuwashuhudia katika mechi za kirafiki na Ngao ya Jamii.

Yanga ndiyo inayotarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa katika kikosi chake kutokana na usajili mpya ilioufanya na wachezaji iliyowaacha.

Katika usajili wa kuimarisha kikosi msimu huu, Yanga wamesajili nyota 12 ambapo wakimatiafa ni Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Carlos Carlinhos, Yacouba Songne na Michael Sarpong.

Wazawa ni Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Zawadi Mauya, Farid Mussa na Wazir Junior.

Kwa upande wa Simba, imesajili nyota wachache kulingana na ubora wa wachezaji wao wa msimu uliopita hivyo haikuwaacha wengi.

Wachezaji wapya watakaovaa jezi ya Msimbazi msimu huu ni Joash Onyango, Larry Bwalya, Chrispine Mugalu, Bernard Morrison, David Kameta ‘Duchu’, Ibrahim Ame na Charles Ilamfya.

Usajili huo mpya wa timu zote ndiyo unaozifanya mechi hizi za mwanzo wa ligi kuwa za kuvuta mashabiki wengi uwanjani, kila mmoja akitaka kushuhudia uwajibikaji wa wachezaji wapya.

Kati ya wachezaji ambao watatazamwa zaidi na mashabiki kwa upande wa Yanga ni Carlinhos, Farid Mussa, Mukoko na Sarpong.

Huko Simba, kuna uwezekano mkubwa wa Morrison, Bwalya na Onyango kuanza kikosi cha kwanza.

Hata hivyo timu hizo zinatarajia kukutana na upinzani mkali kutoka kwa timu mpinzani ambao wataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa kutokana na wasifu wa timu hizo kongwe.

Ihefu FC licha ya kuwa timu ngeni Ligi Kuu Bara, bila shaka haitakubali kuwa kibonde mbele ya Simba ukizingatia ipo uwanja wa nyumbani ikicheze mbele ya halaiki ya mashabiki wake.

Simba inashuka dimbani ikiwa imetoka kushinda taji la Ngao ya Jamii ikiifunga Namungo FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Baada ya mchezo huo Simba ilicheza na Arusha FC katika uwanja huo huo na kuitandika mabao 6-0 hali inayoongeza morali kwa nyota wake.

Yanga nayo imecheza michezo kadhaa ya kirafiki mkubwa ukiwa dhidi ya Aigle Noir ya Burundi na kushinda 2-0 wakati wa kilele cha Wiki ya Wananchi kwenye Uwanja wa Mkapa.

Matokeo ya timu hizo leo, ndiyo yatatoa taswira ya vifaa vyao vipya kuwa vinaweza au ndio wameuziwa mbuzi kwenye gunia.

The post KUMEKUCHAAA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *