Posted By Posted On

MRITHI WA SENZO SIMBA HUYU HAPA, on September 6, 2020 at 12:41 pm

NA ASHA KIGUNDULA BODI ya Wakurugenzi klabu ya Simba, imemtangaza Ofisa Mtendaji Mkuu mpya (CEO), Barbara Gonzalez, kuziba nafasi ya Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini aliyehudumu kwa msimu mmoja kabla ya kujiunga na watani wao Yanga alikopewa nafasi ya kuwa mshauri wa klabu hiyo. Uteuzi huo wa Barbara unamfanya kuwa CEO wa kwanza wa
The post MRITHI WA SENZO SIMBA HUYU HAPA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA ASHA KIGUNDULA

BODI ya Wakurugenzi klabu ya Simba, imemtangaza Ofisa Mtendaji Mkuu mpya (CEO), Barbara Gonzalez, kuziba nafasi ya Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini aliyehudumu kwa msimu mmoja kabla ya kujiunga na watani wao Yanga alikopewa nafasi ya kuwa mshauri wa klabu hiyo.

Uteuzi huo wa Barbara unamfanya kuwa CEO wa kwanza wa kike ndani za klabu hiyo kongwe, akianza kazi rasmi msimu wa 2020/21.

Kabla ya uteuzi huo, bosi huyo mpya alikuwa ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’, pia aliwahi kufanya kazi kama msaidizi wa Senzo wakati akiwa CEO wa Simba.

Kwa mujibu wa wasifu uliotolewa na klabu ya Simba, inaonyesha mwaka 2016, Barbara aliongoza Asasi ya Mo Dewji Foundation inayojihusisha na mambo ya kusaidia Watanzania wasiojiweza katika masuala ya afya, elimu na maendeleo jamii.

Pia aliwahi kufanya kazi katika Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Uongozi cha Vijana wa Afrika (YALI) ukanda wa Afrika Mashariki.

Bodi hiyo ilizinduliwa na aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, ikihusika na juhudi za kuwekeza katika kizazi kijacho cha viongozi wa Kiafrika.

Eneo lingine alilowahi kufanya kazi CEO huyo mpya wa Simba ni ushauri katika Taasisi ya Deloitte Consulting Limited Tanzania inayohusika na miradi ya wateja wa sekta za umma pamoja na mashirika ya kimataifa USAID, UNICEF na Benki ya Dunia.

Kwa upande wa elimu, Barbara ana shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Maendeleo aliyoipata mwaka 2012/13 katika Chuo cha Uchumi na Sayansi ya Siasa ya jijini London nchini Uingereza.

Alisoma shahada yake ya kwanza mwaka 2009-2012 katika masuala ya uchumi na Sayansi ya Siasa katika Chuo cha Manhattanville nchini Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, MO alisema Barbara alipitishwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoketi juzi na kutoa baraka zote.

Alisema wamempa nafasi hiyo baada ya kuona utendaji wake mara baada ya kukabidhiwa mikoba ya Senzo muda mfupi tu alipotimka klabu hapo.

“Bodi ya Wakurugenzi Simba kwa pamoja imeridhishwa na utendaji wake na tumeamua kumpitisha kushika wadhifa huo,” alisema MO.

Akizungumzia uteuzi huo, Barbara alisema ana matumaini makubwa na Simba, wapenzi na wanachama hivyo watarajie mambo mazuri kutoka kwake.

Alisema kufanya kwake vizuri kutaendana na ushirikiano kutoka kwa menejimenti nzima ya Simba.

“Nina matumaini makubwa na Simba, ikiwa ni pamoja na kuchukua mataji yote kama ilivyokuwa msimu uliopita,” alisema.

Uteuzi huo unakuja wakati leo timu ya Simba inafungua pazia la Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 kwa kucheza na Ihefu FC katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

The post MRITHI WA SENZO SIMBA HUYU HAPA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *