Posted By Posted On

MSERBIA WA YANGA APEWA MAJUKUMU MAZITO, on September 6, 2020 at 4:08 am

 KOCHA Mkuu mpya wa Yanga Mserbia, Zlatko Krmpotic amepewa masharti makubwa kwenye mkataba ambayo anatakiwa kuyafanya msimu ujao unaoanza leo Septemba 6. Kocha huyo alitua Jumamosi iliyopita tayari ameanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho kilichoweka kambi yake kwenye Kijiji cha Avic Town huko Kigamboni na leo anaanza kukaa benchi kwa mara ya kwanza wakati timu hiyo itakapovaana na Prisons Uwanja wa Mkapa jijini Dar. Habari zinaeleza kuwa kwenye mkataba wa kocha huyo wa miaka miwili aliousaini amewekewa malengo ambayo ili aendelee kubakia, ni lazima achukue mataji yote watakayoshiriki timu hiyo.Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kati ya mataji hayo, la Ligi Kuu Bara ndiyo limepewa kipaumbele lengo ni kuhakikisha wanawapoka watani wao wa jadi, Simba pamoja na FA. “Kocha mpya Zlatko ana kibarua kigumu katika msimu huu, hiyo ni kutokana na mkataba wake aliousaini ambao unamtaka achukue mataji yote watakayoshiriki Yanga.“Hivyo, kama anataka kuendelea kubakia Yanga basi aipe mataji timu hiyo na kati ya taji ambalo wanalitaka la ubingwa wa ligi ambalo GSM ndio wanalitaka zaidi,” kilisema chanzo hicho.Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga ambaye pia ni Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said alisema: “GSM tumechukua dhamana yote ya msimu huu ya kuhakikisha tunauchukua ubingwa wa ligi, hiyo ndiyo sababu tumebeba dhamana ya kusimamia usajili wote wa msimu huu kwa kuhakikisha tunasajili wachezaji waliokuwa  bora wataoipa ubingwa Yanga.”,


 KOCHA Mkuu mpya wa Yanga Mserbia, Zlatko Krmpotic amepewa masharti makubwa kwenye mkataba ambayo anatakiwa kuyafanya msimu ujao unaoanza leo Septemba 6.

 

Kocha huyo alitua Jumamosi iliyopita tayari ameanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho kilichoweka kambi yake kwenye Kijiji cha Avic Town huko Kigamboni na leo anaanza kukaa benchi kwa mara ya kwanza wakati timu hiyo itakapovaana na Prisons Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

Habari zinaeleza kuwa kwenye mkataba wa kocha huyo wa miaka miwili aliousaini amewekewa malengo ambayo ili aendelee kubakia, ni lazima achukue mataji yote watakayoshiriki timu hiyo.


Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kati ya mataji hayo, la Ligi Kuu Bara ndiyo limepewa kipaumbele lengo ni kuhakikisha wanawapoka watani wao wa jadi, Simba pamoja na FA.

 

“Kocha mpya Zlatko ana kibarua kigumu katika msimu huu, hiyo ni kutokana na mkataba wake aliousaini ambao unamtaka achukue mataji yote watakayoshiriki Yanga.


“Hivyo, kama anataka kuendelea kubakia Yanga basi aipe mataji timu hiyo na kati ya taji ambalo wanalitaka la ubingwa wa ligi ambalo GSM ndio wanalitaka zaidi,” kilisema chanzo hicho.


Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga ambaye pia ni Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said alisema: “GSM tumechukua dhamana yote ya msimu huu ya kuhakikisha tunauchukua ubingwa wa ligi, hiyo ndiyo sababu tumebeba dhamana ya kusimamia usajili wote wa msimu huu kwa kuhakikisha tunasajili wachezaji waliokuwa  bora wataoipa ubingwa Yanga.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *