Posted By Posted On

YANGA WATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA, on September 6, 2020 at 4:29 am

 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hesabu zao kubwa kwa msimu mpya wa 2020/21 ni kuweza kutwaa kombe la Ligi Kuu Bara ambalo lipo mkononi mwa Simba.Kauli hiyo ya uongozi wa Yanga ni ujumbe kwa Simba ambao nao leo wanaanza kurusha kete ya kwanza kwa kumenyana na Ihefu, Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni. Leo Yanga inatupa kete yake ya kwanza kwenye ligi kwa kumenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.  Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, uongozi wa klabu hiyo umejipanga kikamilifu msimu huu kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambao wameukosa kwa misimu mitatu mfululizo.“Usajili tulioufanya msimu huu sio wa kitoto, umezingatia matakwa yote ya timu, wachezaji wapo katika kiwango kizuri tunachohitaji ni kuona tunafanikiwa kufanya vizuri kwenye ligi na kutwaa ubingwa mwisho wa msimu. “Usajili ambao tumeufanya hatujaufanya katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo, hivyo tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwa kushirikiana na benchi la ufundi, wachezaji na uongozi kwa ujumla ili tupate matokeo mazuri,” amesema Mwakalebela. ,


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hesabu zao kubwa kwa msimu mpya wa 2020/21 ni kuweza kutwaa kombe la Ligi Kuu Bara ambalo lipo mkononi mwa Simba.


Kauli hiyo ya uongozi wa Yanga ni ujumbe kwa Simba ambao nao leo wanaanza kurusha kete ya kwanza kwa kumenyana na Ihefu, Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.

 

Leo Yanga inatupa kete yake ya kwanza kwenye ligi kwa kumenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

 

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, uongozi wa klabu hiyo umejipanga kikamilifu msimu huu kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambao wameukosa kwa misimu mitatu mfululizo.


“Usajili tulioufanya msimu huu sio wa kitoto, umezingatia matakwa yote ya timu, wachezaji wapo katika kiwango kizuri tunachohitaji ni kuona tunafanikiwa kufanya vizuri kwenye ligi na kutwaa ubingwa mwisho wa msimu.

 

“Usajili ambao tumeufanya hatujaufanya katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo, hivyo tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwa kushirikiana na benchi la ufundi, wachezaji na uongozi kwa ujumla ili tupate matokeo mazuri,” amesema Mwakalebela.

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *