Posted By Posted On

AZAM FC WAKIWASHA VPL,WAICHAPA BAO 1-0 POLISI TANZANIA

 KIKOSI cha Azam FC leo Septemba 7 kimefungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania. Mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa uliwafanya matajiri wa Dar es Salaam kusubiri mpaka dakika ya 44 kupachika bao la ushindi.Bao hilo lilipachikwa na mshambuliaji namba moja wa Azam FC, Obrey Chirwa kwa pasi ya Prince Dube.Jitihada za Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini kupambana kuweka usawa ziligonga mwamba mbele ya beki bora wa msimu uliopita, Nocolas Wadada.Azam inayonolewa na Aristica Cioaba inazibakiza pointi zote tatu Chamazi. Inaanza kujiaanda dhidi ya Coastal Union, Septemba 11, Uwanja wa Azam Complex.,

 KIKOSI cha Azam FC leo Septemba 7 kimefungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania. 

Mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa uliwafanya matajiri wa Dar es Salaam kusubiri mpaka dakika ya 44 kupachika bao la ushindi.

Bao hilo lilipachikwa na mshambuliaji namba moja wa Azam FC, Obrey Chirwa kwa pasi ya Prince Dube.

Jitihada za Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini kupambana kuweka usawa ziligonga mwamba mbele ya beki bora wa msimu uliopita, Nocolas Wadada.

Azam inayonolewa na Aristica Cioaba inazibakiza pointi zote tatu Chamazi. Inaanza kujiaanda dhidi ya Coastal Union, Septemba 11, Uwanja wa Azam Complex.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *