Posted By Posted On

KROSI YA PRINCE DUBE, CHIRWA APIGA BAO PEKEE CHAMAZI AZAM FC YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAMBAO pekee la mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.Chirwa alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.Mechi nyingine za leo, KMC iliibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, mabao ya Israel Mwenda, Hassan Kabunda, Abdul Hillary na Paul Peter.Nayo JKT Tanzania ikapata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyej, Kagera Sugar – bao pekee la Adam Adam dakika ya 16 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.,

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BAO pekee la mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Chirwa alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
Mechi nyingine za leo, KMC iliibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, mabao ya Israel Mwenda, Hassan Kabunda, Abdul Hillary na Paul Peter.
Nayo JKT Tanzania ikapata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyej, Kagera Sugar – bao pekee la Adam Adam dakika ya 16 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *