Posted By Posted On

Mapinduzi Queens, Unyanyembe zapanda Ligi Kuu ya Wanawake,, on September 7, 2020 at 6:52 am

NA TIMA SIKILO, DODOMA TIMU ya wanawake ya Mapinduzi Queens ya mkoani Njombe na Unyanyembe ya Tabora, zimefanikiwa kupanda daraja hadi Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2020/21 baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali jana. Mechi hizo zilichezwa jana asubuhi kwenye Uwanja wa Shule ya Fountain Gate Arena, jijini hapa, Mapinduzi,

NA TIMA SIKILO, DODOMA

TIMU ya wanawake ya Mapinduzi Queens ya mkoani Njombe na Unyanyembe ya Tabora, zimefanikiwa kupanda daraja hadi Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2020/21 baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali jana.

Mechi hizo zilichezwa jana asubuhi kwenye Uwanja wa Shule ya Fountain Gate Arena, jijini hapa, Mapinduzi Queens wakiifunga Ever Green ya Dar es Salaam mabao 4-0, huku Unyanyembe wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ilala Queens ya Dar es Salaam.

Mapinduzi Queens walipata ushindi huo kwa mikwaju ya penalti 4-0 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya wapinzani wao hao.

Mabao ya Mapinduzi yalifungwa na Clara Luvanga dakika ya 55, Happy Faustine dakika ya 83 na Halima Moses akifunga la tatu dakika ya 86.

Kwa upande wa Unyanyembe Queens, mabao yao yalifungwa na Ashura Shabani dakika ya saba, Hawa Ramadhan dakika 22 na Sharifa Salum dakika ya 29.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *