Posted By Posted On

SIMBA YATIA TIMU BONGO, KUANZA KUIPIGIA HESABU MTIBWA SUGAR, on September 7, 2020 at 9:22 am

 KIKOSI cha Simba kimewasili leo Dar es Salaam kikitokea Mbeya ambapo kilikuwa na mchezo wa Kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu FC uliochezwa Uwanja wa Sokoine. Simba imetua leo kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyererere.Kwenye mchezo wa jana, Septemba 6, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo yale ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco na lile la pili kiungo Mzamiru Yassin.Bao pekee la wana Ihefu FC lilipachikwa na Omary Mponda aliyefunga bao hilo katikati ya msitu wa mabeki wa tatu wa Simba wakiongozwa na Joash Onyango. Kwa sasa Simba inaanza kujiaandaa kwa ajili ya mchezo wake wa pili Septemba 12 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.,

 KIKOSI cha Simba kimewasili leo Dar es Salaam kikitokea Mbeya ambapo kilikuwa na mchezo wa Kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu FC uliochezwa Uwanja wa Sokoine. 

Simba imetua leo kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyererere.

Kwenye mchezo wa jana, Septemba 6, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo yale ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco na lile la pili kiungo Mzamiru Yassin.

Bao pekee la wana Ihefu FC lilipachikwa na Omary Mponda aliyefunga bao hilo katikati ya msitu wa mabeki wa tatu wa Simba wakiongozwa na Joash Onyango. 

Kwa sasa Simba inaanza kujiaandaa kwa ajili ya mchezo wake wa pili Septemba 12 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *