Posted By Posted On

SIMBA YAUA, LAKINI…,, on September 7, 2020 at 6:43 am

NA MWANDISHI WETU-MBEYA MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wameanza vizuri kampeni yao ya kutetea taji lao hilo jana kwa kuichapa Ihefu mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Hata hivyo, ushindi huo umeonekana kutowafurahisha wapenzi wa timu hiyo ambao walikuwa wakitarajia kutoka uwanjani na mabao zaidi ya matano dhidi ya wapinzani wao,

NA MWANDISHI WETU-MBEYA

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wameanza vizuri kampeni yao ya kutetea taji lao hilo jana kwa kuichapa Ihefu mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Hata hivyo, ushindi huo umeonekana kutowafurahisha wapenzi wa timu hiyo ambao walikuwa wakitarajia kutoka uwanjani na mabao zaidi ya matano dhidi ya wapinzani wao hao waliopanda daraja msimu huu.

Moja ya sababu ambazo zilikuwa zikiwapa jeuri wapenzi wa Simba kuvuna mabao mengi jana, ni kitendo cha kikosi chao kutofanyiwa mabadiliko makubwa, lakini pia wakiwa na wachezaji wanaoamini ni wa kiwango cha juu.

Hata hivyo, hadi dakika 90 za mchezo huo wa jana zinamalizika, Simba walitoka uwanjani na ushindi wa mabao 2-1, wafungaji wakiwa ni nahodha John Bocco na Muzamiri Yassin.

Bao la Ihefu iliyopanda daraja baada ya kuitoa Mbao katika mechi mbili za mtoano (playoff), lilifungwa na mshambuliaji wake, Omary Mponda.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Dar es Salaam, Simba ndiyo walioanza kwa kasi, japo Ihefu nao walionekana kutotishwa na ukubwa wa jina la wapinzani wao hao.

Baada ya mashambulizi kadhaa, hatimaye Simba ilipata bao la kwanza dakika ya 10 kupitia kwa Bocco, akiitumia vema pasi murua ya Mzamiru.

Bao hilo lilionekana kuwazindua Ihefu waliokuja juu na kufanya mashambulizi langoni mwa Simba ambayo hata hivyo yalizimwa na beki wa kati wa Wekundu wa Msimbazi hao, Joash Onyango.

Lakini dakika ya 14, Mponda aliisawazishia Ihefu kwa shuti kali la chini chini lililomshinda mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula na mpira kwenda nyavuni.

Dakika ya 16, mlinda malango wa Ihefu, Andrew Kayuni, alifanya kazi ya ziada kupangua mchomo hatari uliopigwa na beki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tashabalala’ na kuzaa kona ambayo hata hivyo, haikuzaa matunda.

Dakika ya 19, nusura Enock Jiah aindikie Ihefu bao la pili baada ya kuachia shuti kali lililopanguliwa na Manula na kuzaa kona tasa.

Dakika ya 30, Bocco alipoteza nafasi ya wazi ya kuiandikia Simba bao la pili baada ya kupiga mpira kwa kichwa uliotua mikononi mwa kipa wa Ihefu.

Dakika chache baadaye, Jiah akiwa katika nafasi nzuri, aliikosesha Ihefa bao baada ya kupiga shuti hafifu lililodakwa na Manula kiulaini.

Dakika tatu kabla ya mapumziko, Muzamiru aliifungia Simba bao la pili kwa kichwa, akimalizia mpira uliopigwa na Clatous Chama aliyepokea krosi safi akiwa pembeni ya uwanja kutoka wka Hassan Dilunga.

Dakika ya 44, mlinzi wa kushoto wa Ihefu, Emmauel Kichiba, alilimwa kadi ya njano baada ya kuchezea rafu Chama kabla ya Dilunga kuonyeshwa kadi kama hiyo dakika ya 45 kutokana na kumfanyia madhambi Kichiba.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika, Simba wakiwa mbele kwa mabao 2-1. 

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kupania kupata mabao zaidi, Simba wakitaka kuongeza, huku Ihefu wakipiga hesabu za kusawazisha na kujipatia ya mengine ya ushindi.

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, dakika ya 82, nusura aindikie Simba bao la tatu, lakini shuti lake lilizuiliwa na walinzi wa Ihefu.

Dakika ya 87, Manula alifanya kazi ya ziada kupangua hatari langoni mwake baada ya shambulizi la kushtukiza lililofanywa na Ihefu.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika Uwanja wa Sokoine kwa Simba kutoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefa FC.

KIKOSI CHA IHEFA: Andrew Kayuni, Omaru Kondamba, Emanuel Kichiba, Godfrey Rafael, Michael Masinda, Sudi Mlindwa, Jordan John, Willu Mgaya, Joseph Kinyozi, Omary Mponda na Enock Jiah.

KIKOSI CHA SIMBA: Aishi Manula, Shomaru Kapombe, Onyango, Kenney Juma, JonaS Mkude, Hassan Dilunga/Ibrahim Ajib (dk.62), Mzamiru Yassin, John Bocco, Claotus Chama na Bernard Morrison/Meddie Kagere (dk.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *