Posted By Posted On

YANGA YAPIGA HESABU YA KUKUSANYA MATAJI MSIMU MPYA WA 2020/21, on September 7, 2020 at 6:35 am

 BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema kutokana na ubora wa kikosi cha wachezaji walichonacho anapata uhakika wa kubeba makombe katika msimu ujao, Ligi Kuu Bara pamoja na michuano mingine watakayoshiriki. Ninja ambaye ameanza kucheza sambamba na beki mpya wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto ametoa kauli hiyo kufuatia kuwa na muunganiko mzuri kwa wachezaji wa kikosi hicho. Ninja amesema kuwa, umefika wakati kwa mashabiki wa timu hiyo kuanza kupata furaha ya makombe kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kwani uongozi wa timu hiyo umefanya mabadiliko makubwa ya kiufundi. “Ukweli naona tumekuwa na timu nzuri ambayo italeta ushindani na jambo kubwa kwetu wachezaji ni kuweza kujituma ili kufikia malengo na nitacheza na mchezaji yeyote ambaye nitapangwa naye kwa sababu tunataka kufikia malengo ya pamoja. “Ndoto kubwa kwa mashabiki ni kupata makombe ndiyo jambo ambalo kwao wamekuwa na kiu nalo katika kipindi kirefu, binafsi naamini kwa timu ambayo tupo nayo basi wajiandae kuyapokea makombe japo tunatambua ushindani wa ligi utakuwa mkubwa lakini kwa umoja wetu tutafanikiwa,” amesema Ninja.Jana Yanga ilianza kutupa kete yake ya kwanza Uwanja wa Mkapa mbele ya Tanzania Prisons na zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.,


 BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema kutokana na ubora wa kikosi cha wachezaji walichonacho anapata uhakika wa kubeba makombe katika msimu ujao, Ligi Kuu Bara pamoja na michuano mingine watakayoshiriki.

 

Ninja ambaye ameanza kucheza sambamba na beki mpya wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto ametoa kauli hiyo kufuatia kuwa na muunganiko mzuri kwa wachezaji wa kikosi hicho.


 Ninja amesema kuwa, umefika wakati kwa mashabiki wa timu hiyo kuanza kupata furaha ya makombe kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kwani uongozi wa timu hiyo umefanya mabadiliko makubwa ya kiufundi.

 

“Ukweli naona tumekuwa na timu nzuri ambayo italeta ushindani na jambo kubwa kwetu wachezaji ni kuweza kujituma ili kufikia malengo na nitacheza na mchezaji yeyote ambaye nitapangwa naye kwa sababu tunataka kufikia malengo ya pamoja.

 

“Ndoto kubwa kwa mashabiki ni kupata makombe ndiyo jambo ambalo kwao wamekuwa na kiu nalo katika kipindi kirefu, binafsi naamini kwa timu ambayo tupo nayo basi wajiandae kuyapokea makombe japo tunatambua ushindani wa ligi utakuwa mkubwa lakini kwa umoja wetu tutafanikiwa,” amesema Ninja.


Jana Yanga ilianza kutupa kete yake ya kwanza Uwanja wa Mkapa mbele ya Tanzania Prisons na zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *