Posted By Posted On

ASTON VILLA YAIWINDA SAINI YA MSHAMBULIAJI OLLIE

KLABU ya Aston Villa ipo kwenye mchakato wa kukamilisha usajili wa kuipata saini ya mshambuliaji wa Brentford, Ollie Watkins ambaye awali dau lake lilitajwa kuwa ni pauni milioni 28.Ikiwa Villa watapa saini ya mshambuliaji huyo itavunja benki na kutoa mkwanja mrefu kupata saini ya mshambuliaji huyo ambaye thamani yake inatajwa kuwa inaweza kupanda mpaka pauni milioni 33.Kocha Mkuu wa Aston Villa, Dean Smith anahitaji kuboresha kikosi chake hasa kwenye safu ya ushambuliaji  na yupo tayari kutoa dau la pauni milioni 28 kupata saini ya mchezaji huyo.Nyota huyo alifunga jumla ya mabao 26 kwenye mashindano yote msimu uliopita pia amezivutia timu nyingine ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ambazo ni pamoja na Tottenham, Crystal Palace na West Ham.Mpango mkubwa ni kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo pia inaundwa na Mtanzania, Mbwana Samatta ambaye alijiunga na klabu hiyo Januari akitokea Genk ya Ubelgiji.Samatta ameshindwa kwenda na kasi ya Ligi Kuu England ambapo licha ya kusajiliwa kwa dau la pauni milioni 8 ameweza kufunga mabao mawili pekee jambo linalompa wakati mgumu Smith kwenye upande wa safu ya ushambuliaji.,


KLABU ya Aston Villa ipo kwenye mchakato wa kukamilisha usajili wa kuipata saini ya mshambuliaji wa Brentford, Ollie Watkins ambaye awali dau lake lilitajwa kuwa ni pauni milioni 28.

Ikiwa Villa watapa saini ya mshambuliaji huyo itavunja benki na kutoa mkwanja mrefu kupata saini ya mshambuliaji huyo ambaye thamani yake inatajwa kuwa inaweza kupanda mpaka pauni milioni 33.

Kocha Mkuu wa Aston Villa, Dean Smith anahitaji kuboresha kikosi chake hasa kwenye safu ya ushambuliaji  na yupo tayari kutoa dau la pauni milioni 28 kupata saini ya mchezaji huyo.

Nyota huyo alifunga jumla ya mabao 26 kwenye mashindano yote msimu uliopita pia amezivutia timu nyingine ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ambazo ni pamoja na Tottenham, Crystal Palace na West Ham.


Mpango mkubwa ni kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo pia inaundwa na Mtanzania, Mbwana Samatta ambaye alijiunga na klabu hiyo Januari akitokea Genk ya Ubelgiji.


Samatta ameshindwa kwenda na kasi ya Ligi Kuu England ambapo licha ya kusajiliwa kwa dau la pauni milioni 8 ameweza kufunga mabao mawili pekee jambo linalompa wakati mgumu Smith kwenye upande wa safu ya ushambuliaji.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *