Posted By Posted On

KAGERE AFIKIRIA KUWEKA REKODI NYINGINE NDANI YA LIGI KUU BARA

 MEDDIE Kagere, mtupiaji namba moja wa muda wote kwa misimu miwili mfululizo ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa bado ana malengo ya kuendelea kufunga mabao katika Ligi Kuu Bara licha ya kuwepo na ushindani ndani ya kikosi chake.Kagere raia wa Rwanda ametupia jumla ya mabao 45 ndani ya ardhi ya Bongo kwenye Ligi Kuu Bara ambapo msimu wa 2018/19 alitupia 23 na msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22.Kagere, amesema kuwa anachokiangalia kwa sasa ni kuona namna gani anaweza kuifikia rekodi yake ya msimu uliopita katika ufungaji.”Natamani kuona kwamba ninaifikia rekodi yangu ya msimu uliopita kwa sababu ndio itasaidia katika timu kupata mafanikio ya kutetea ubingwa.”Kikubwa kwangu kwa sasa ni kujitoa kwa ajili ya kutimiza majukumu yangu ndani ya timu kwa kuhakikisha timu inapata matokeo chanya,” amesema.Ingizo jipya Chris Mugalu, Charles Ilanfya ni miongoni mwa nyota watakaokuwa wakigombania namba na nyota huyo ambaye anakubali uwezo wa mshambuliaji mwenzake John Bocco.,

 


MEDDIE Kagere, mtupiaji namba moja wa muda wote kwa misimu miwili mfululizo ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa bado ana malengo ya kuendelea kufunga mabao katika Ligi Kuu Bara licha ya kuwepo na ushindani ndani ya kikosi chake.

Kagere raia wa Rwanda ametupia jumla ya mabao 45 ndani ya ardhi ya Bongo kwenye Ligi Kuu Bara ambapo msimu wa 2018/19 alitupia 23 na msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22.

Kagere, amesema kuwa anachokiangalia kwa sasa ni kuona namna gani anaweza kuifikia rekodi yake ya msimu uliopita katika ufungaji.

“Natamani kuona kwamba ninaifikia rekodi yangu ya msimu uliopita kwa sababu ndio itasaidia katika timu kupata mafanikio ya kutetea ubingwa.

“Kikubwa kwangu kwa sasa ni kujitoa kwa ajili ya kutimiza majukumu yangu ndani ya timu kwa kuhakikisha timu inapata matokeo chanya,” amesema.

Ingizo jipya Chris Mugalu, Charles Ilanfya ni miongoni mwa nyota watakaokuwa wakigombania namba na nyota huyo ambaye anakubali uwezo wa mshambuliaji mwenzake John Bocco.,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *