Posted By Posted On

KOCHA MRUNDI AKUBALI MUZIKI WA KISINDA,AMTABIRIA MAKUBWA

 KOCHA Mkuu wa Aigle Noir ya Burundi, Gustave Niyonkuru, amevutiwa na kiwango kilichooneshwa na kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mkongomani, Tuisila Kisinda. Kisinda ni ingizo jipya ndani ya Yanga akitokea Klabu ya AS Vita, amekuwa na kasi ndani ya uwanja huku wengi wakimtabiria kufanya makubwa msimu huu.Kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi, Kisinda alipachika bao moja wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 mbele ya timu hiyo Uwanja wa Mkapa.Niyonkuru amesema:“Nimevutiwa na yule aliyekuwa akishambulia kutokea pembeni na kufanikiwa kufunga bao la kwanza, wanamwita Kisinda, ni mchezaji mzuri na kwa kweli atawasaidia sana Yanga.”Kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Kisinda aliweza kufanya majaribio hatari matatu ambayo hayakuzaa matunda.Kwenye mchezo huo uliochezwa Septemba 6, Yanga ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na bao la Yanga lilipachikwa na Michael Sarpong.,


 KOCHA Mkuu wa Aigle Noir ya Burundi, Gustave Niyonkuru, amevutiwa na kiwango kilichooneshwa na kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mkongomani, Tuisila Kisinda.

 

Kisinda ni ingizo jipya ndani ya Yanga akitokea Klabu ya AS Vita, amekuwa na kasi ndani ya uwanja huku wengi wakimtabiria kufanya makubwa msimu huu.


Kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi, Kisinda alipachika bao moja wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 mbele ya timu hiyo Uwanja wa Mkapa.


Niyonkuru amesema:“Nimevutiwa na yule aliyekuwa akishambulia kutokea pembeni na kufanikiwa kufunga bao la kwanza, wanamwita Kisinda, ni mchezaji mzuri na kwa kweli atawasaidia sana Yanga.”


Kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Kisinda aliweza kufanya majaribio hatari matatu ambayo hayakuzaa matunda.


Kwenye mchezo huo uliochezwa Septemba 6, Yanga ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na bao la Yanga lilipachikwa na Michael Sarpong.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *