Posted By Posted On

MBAPPE AKUTWA NA COVID 19, KUKOSEKANA LEO UFARANSA NA CROATIA

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe jana alipimwa na kukutwa na ugonjwa wa COVID-19 na atakosekana kwenye kikosi cha Ufaransa leo kikimenyana na Croatia katika mchezo wa Kundi la Tatu Ligi ya Mataifa Ulaya Uwanja wa Stade de France Jijini Paris.Mbappe aliyefunga bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Sweden 1-0 Jumamosi, hilo likiwa bao lake la 14 kwenye timu yake ya taifa – alirudishwa nyumbani jana.Shirikisho limesema Mbappe alifuzu vipimo vya awali kabla ya kuungana na wachezaji wenzake mazoezini na akafuzu pia vipimo vya pili Jumatano iliyopita kuelekea mechi na Sweden. Kylian Mbappe atakosekana leo Ufaransa ikimenyana Croatia Ligi ya Mataifa Ulaya Uwanja wa Stade de France Jijini Paris PICHA ZAIDI GONGA HAPA,

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe jana alipimwa na kukutwa na ugonjwa wa COVID-19 na atakosekana kwenye kikosi cha Ufaransa leo kikimenyana na Croatia katika mchezo wa Kundi la Tatu Ligi ya Mataifa Ulaya Uwanja wa Stade de France Jijini Paris.
Mbappe aliyefunga bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Sweden 1-0 Jumamosi, hilo likiwa bao lake la 14 kwenye timu yake ya taifa – alirudishwa nyumbani jana.
Shirikisho limesema Mbappe alifuzu vipimo vya awali kabla ya kuungana na wachezaji wenzake mazoezini na akafuzu pia vipimo vya pili Jumatano iliyopita kuelekea mechi na Sweden. 


Kylian Mbappe atakosekana leo Ufaransa ikimenyana Croatia Ligi ya Mataifa Ulaya Uwanja wa Stade de France Jijini Paris PICHA ZAIDI GONGA HAPA

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *