Posted By Posted On

IHEFU FC KUIVAA RUVU SHOOTING IKIWA NA MAJEMBE YAKE YA KAZI MAPYA

IHEFU FC yeye maskani yake Mbeya, ina kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting, Septemba 13 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.Itaingia uwanjani ikiwa na kumbukukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza Septemba 6 kwa kuchapwa mabao 2-1 mbele ya Simba Uwanja wa Sokoine.Kazi kubwa itakuwa ni kusaka ushindi wao wa kwanza mbele ya Ruvu Shooting ambao wao wametoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Gairo, Septemba 6.Inaingia ndani ya uwanja ikiwa imemalizana na baadhi ya nyota wake waliokuwa ndani ya kikosi hicho kilichopanda Ligi Kuu Bara msimu huu pamoja na wachezaji wengine wapya ambao ni pamoja na :-Geoffrey Raphael Kivywanzi ambaye walinasa saini yake akitokea timu ya Mbeya Kwanza alitambulishwa Agosti 17. Pia Agosti 17 mshambuliaji wao ambaye ni kapteni, Joseph Kinyozi aliongeza dili la kubaki ndani ya Ihefu. Agosti 18, mshambuliaji, Jordan John alisaini Ihefu akitokea Klabu ya Mbao FC. Agosti 18 beki wa kati Wema Sadoki alisaini mkataba wa kuitumikia timu ya Ihefu alitokea Klabu ya Alliance FC. Agosti 18, Kiungo wao, Willy Mgaya aliongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo. Agosti 19, mshambuliaji, Paul Materaz Luyungu alisaini mkataba wa kuichezea timu ya Ihefu FC akitokea Klabu ya Lipuli. Agosti 20, kiungo Omary Khamis alisaini mkataba wa kuitumikia timu ya Ihefu akitokea timu ya Ndanda FC.,


IHEFU FC yeye maskani yake Mbeya, ina kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting, Septemba 13 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Itaingia uwanjani ikiwa na kumbukukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza Septemba 6 kwa kuchapwa mabao 2-1 mbele ya Simba Uwanja wa Sokoine.


Kazi kubwa itakuwa ni kusaka ushindi wao wa kwanza mbele ya Ruvu Shooting ambao wao wametoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Gairo, Septemba 6.


Inaingia ndani ya uwanja ikiwa imemalizana na baadhi ya nyota wake waliokuwa ndani ya kikosi hicho kilichopanda Ligi Kuu Bara msimu huu pamoja na wachezaji wengine wapya ambao ni pamoja na :-Geoffrey Raphael Kivywanzi ambaye walinasa saini yake akitokea timu ya Mbeya Kwanza alitambulishwa Agosti 17.

Pia Agosti 17 mshambuliaji wao ambaye ni kapteni, Joseph Kinyozi aliongeza dili la kubaki ndani ya Ihefu.

Agosti 18, mshambuliaji, Jordan John alisaini Ihefu akitokea Klabu ya Mbao FC.

Agosti 18 beki wa kati Wema Sadoki alisaini mkataba wa kuitumikia timu ya Ihefu alitokea Klabu ya Alliance FC.

Agosti 18, Kiungo wao, Willy Mgaya aliongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo.

Agosti 19, mshambuliaji, Paul Materaz Luyungu alisaini mkataba wa kuichezea timu ya Ihefu FC akitokea Klabu ya Lipuli.

Agosti 20, kiungo Omary Khamis alisaini mkataba wa kuitumikia timu ya Ihefu akitokea timu ya Ndanda FC.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *