Posted By Posted On

LYANGA WA AZAM FC ACHEKELEA KUWA SEHEMU YA MAFANIKIO

 AYOUB Lyanga nyota mpya ndani ya Klabu ya Azam FC amesema kuwa anafurahi kuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi chake kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 7.Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, raundi ya kwanza.Lyanga ni ingizo jipya ambapo ameibukia ndani ya kikosi hicho cha matajiri wa Dar es Salaam akitokea Klabu ya Coastal Union yenye maskani yake Tanga.Bao la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 44 kwa pasi ya Prince Dube lilidumu mpaka mwisho wa dakika 90 kwa nyota wa Polisi Tanzania kukwama kumtungua David Kissu. Lyanga amesema:-“Ni furaha kuwa ndani ya timu ambayo ina mipango mizuri, ninafurahi kuona sapoti kutoka kwa mashabiki pamoja na namna timu inavyoelewana uwanjani, ” amesema. Mchezo unaofuata kwa Azam FC ni dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Chamazi, Septemba 11 majira ya saa 1:00 usiku.Azam FC inakutana na Coastal Union iliyo chini ya Juma Mgunda ikiwa imetoka kupoteza pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Namungo FC, Uwanja wa Majaliwa,Lindi.,

 

AYOUB Lyanga nyota mpya ndani ya Klabu ya Azam FC amesema kuwa anafurahi kuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi chake kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 7.


Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, raundi ya kwanza.


Lyanga ni ingizo jipya ambapo ameibukia ndani ya kikosi hicho cha matajiri wa Dar es Salaam akitokea Klabu ya Coastal Union yenye maskani yake Tanga.


Bao la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 44 kwa pasi ya Prince Dube lilidumu mpaka mwisho wa dakika 90 kwa nyota wa Polisi Tanzania kukwama kumtungua David Kissu. 


Lyanga amesema:-“Ni furaha kuwa ndani ya timu ambayo ina mipango mizuri, ninafurahi kuona sapoti kutoka kwa mashabiki pamoja na namna timu inavyoelewana uwanjani, ” amesema. 


Mchezo unaofuata kwa Azam FC ni dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Chamazi, Septemba 11 majira ya saa 1:00 usiku.


Azam FC inakutana na Coastal Union iliyo chini ya Juma Mgunda ikiwa imetoka kupoteza pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Namungo FC, Uwanja wa Majaliwa,Lindi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *