Posted By Posted On

DYBALA HAONDOKI JUVENTUS

IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Juventus ina mpango wa kumpatia mkataba mpya wa miaka mitano staa wake, Paulo Dybala. Mkataba wa awali ya Dybala ndani ya Juventus unatarajiwa kumalizika Juni 2022 baada ya kuusaini mwaka 2017.   Juventus wanataka kumuongeza straika huyo mkataba kutokana na ubora ndani ya timu hiyo na amekuwa kati ya wachezaji tegemeo.   Dybala ambaye msimu uliopita aliibuka kuwa mchezaji bora ndani ya Serie A, pia  aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kuifikisha timu yake hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.   Ripoti zinaeleza kuwa, Mkurugenzi wa Ufundi wa Juventus, Fabio Paratici yupo kwenye mazungumzo na wakala wa Dybala Jorge Antun kwa ajili ya mkataba mpya. Uongozi wa klabu hiyo una mpango wa kumpatia mkataba wa miaka mitano kwa maana hiyo Dybala atakuwa ni mchezaji wa pili kulipwa vizuri ndani ya kikosi hicho baada ya Cristiano Ronaldo. Dybala atakuwa analipwa kiasi cha euro 7m kwa msimu na euro 10m kama bonasi ndani ya kikosi hicho.   Juventus inataka kukamilisha dili hilo baada ya Klabu za Man United, PSG na Real Madrid kuonekana kusaka saini ya mchezaji huyo.,

IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Juventus ina mpango wa kumpatia mkataba mpya wa miaka mitano staa wake, Paulo Dybala.

Mkataba wa awali ya Dybala ndani ya Juventus unatarajiwa kumalizika Juni 2022 baada ya kuusaini mwaka 2017.

 

Juventus wanataka kumuongeza straika huyo mkataba kutokana na ubora ndani ya timu hiyo na amekuwa kati ya wachezaji tegemeo.

 

Dybala ambaye msimu uliopita aliibuka kuwa mchezaji bora ndani ya Serie A, pia  aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kuifikisha timu yake hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Ripoti zinaeleza kuwa, Mkurugenzi wa Ufundi wa Juventus, Fabio Paratici yupo kwenye mazungumzo na wakala wa Dybala Jorge Antun kwa ajili ya mkataba mpya.

Uongozi wa klabu hiyo una mpango wa kumpatia mkataba wa miaka mitano kwa maana hiyo Dybala atakuwa ni mchezaji wa pili kulipwa vizuri ndani ya kikosi hicho baada ya Cristiano Ronaldo.


Dybala atakuwa analipwa kiasi cha euro 7m kwa msimu na euro 10m kama bonasi ndani ya kikosi hicho.

 

Juventus inataka kukamilisha dili hilo baada ya Klabu za Man United, PSG na Real Madrid kuonekana kusaka saini ya mchezaji huyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *