Posted By Posted On

HESABU ZA KAGERA SUGAR KWA YANGA BADO KABISA

 MECKY Mexime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wanaanza kumalizana kwanza na Gwambina Septemba 11 kisha Yanga itafuata Septemba 19. Mexime amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa ndani ya Ligi Kuu Bara ila hesabu zao ni kuona wanafikia malengo waliyojiweka ya kupata pointi tatu.“Mchezo wetu uliopita tumeachana nao sasa tunaipigia hesabu Gwambina, tupo vizuri na tukishamalizana na hawa Gwambina ndipo tutarudi Kaitaba kwa ajili ya kuanza kujiaandaa dhidi ya Yanga.”Ligi ni ngumu hilo lipo wazi kwa kuwa kila timu ilipata muda wa kujiaanaa na kufanya usajili. Bado kuna muda ambao tunahitaji kuunganisha timu ukizingatia kwamba hatukuwa na muda mrefu wa mazoezi kutokana na janga la Virusi vya Corona kuwa sababu a haya yote,” amesema Mexime.Kagera Sugar ilifungua pazia la ligi kwa kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Septemba 7, Uwanja wa Kaitaba. Itakutana na Gwambina ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Biashara United. ,


 MECKY Mexime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wanaanza kumalizana kwanza na Gwambina Septemba 11 kisha Yanga itafuata Septemba 19.

 Mexime amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa ndani ya Ligi Kuu Bara ila hesabu zao ni kuona wanafikia malengo waliyojiweka ya kupata pointi tatu.

“Mchezo wetu uliopita tumeachana nao sasa tunaipigia hesabu Gwambina, tupo vizuri na tukishamalizana na hawa Gwambina ndipo tutarudi Kaitaba kwa ajili ya kuanza kujiaandaa dhidi ya Yanga.


“Ligi ni ngumu hilo lipo wazi kwa kuwa kila timu ilipata muda wa kujiaanaa na kufanya usajili. Bado kuna muda ambao tunahitaji kuunganisha timu ukizingatia kwamba hatukuwa na muda mrefu wa mazoezi kutokana na janga la Virusi vya Corona kuwa sababu a haya yote,” amesema Mexime.

Kagera Sugar ilifungua pazia la ligi kwa kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Septemba 7, Uwanja wa Kaitaba. Itakutana na Gwambina ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Biashara United.

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *