Posted By Posted On

HII HAPA NI REKODI MATATA YA YANGA BONGO, HAIJAWAHI KUTOKEA MISIMU TISA

HII ni rekodi mpya ya Yanga ambayo imejirudia baada ya kupita takribani misimu kumi ndani ya Ligi Kuu Bara.   Yanga ambayo ilianzishwa mwaka 1935, ndiyo mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara baada ya kulitwaa mara 27, wakifuatiwa na Simba wenye mataji 21.   Wikiendi iliyopita ambapo Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ilianza, ndiyo Yanga iliweka rekodi hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Prisons kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.   Rekodi ambayo Yanga imeiweka ni ya kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi ya kwanza ya ligi kwa msimu wa pili mfululizo. Awali iliwahi kufanya hivyo katika msimu wa 2011/12 na 2012/13. Kisha haijawahi kujirudia hadi msimu huu.   Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita, Yanga ilianza kwa kupokea kichapo kutoka kwa Ruvu Shooting cha bao 1-0, msimu huu ikatoka sare ya 1-1 na Priosons.   Katika msimu wa 2011/12, Yanga ikiwa nyumbani, ilianza ligi kwa kufungwa Yanga 0-1 JKT Ruvu ambayo kwa sasa ni JKT Tanzania, kisha 2012/13 ikatoka 0-0 na Prisons ugenini.   Msimu wa 2019/20, Yanga ilifungwa na Ruvu Shooting bao 1-0, kisha msimu huu ikatoka sare ya 1-1 na Prisons. Mechi hizo zote Yanga ilikuwa nyumbani.   Wakati Yanga ikianza msimu wa 2011/12 kwa kipigo, ilimaliza ligi nafasi ya tatu ikikusanya pointi 49. Mabingwa walikuwa Simba waliokusanya pointi 62, nafasi ya pili ilishikwa na Azam iliyokuwa na pointi 56.   Msimu wa 2012/13, Yanga licha ya kuanza kwa sare, lakini ilikuwa bingwa kwa kukusanya pointi 60. Nafasi ya pili ilishikwa na Azam iliyokuwa na pointi 54 na Simba ya tatu ikiwa na pointi 45.   2019/20, Yanga ilipofungwa mechi ya kwanza, ilimaliza ligi nafasi ya pili ikiwa na pointi 72 katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Simba waliokusanya pointi 88.   Msimu huu imeanza kwa sare, kitakachotokea mwisho wa msimu kila mmoja anakisubiri kama kitajirudia kile kilichotokea msimu wa 2012/13.   Ukiangalia katika rekodi hizo, Yanga ilicheza na timu zote za majeshi ambazo ni JKT Tanzania, Ruvu Shooting na Prisons mara mbili.   KOCHA ZLATKO ASHANGAA Baada ya kuanza ligi kwa sare, mashabiki wa timu hiyo walianza kutoa maneno mengi juu ya kikosi chao hicho ambapo Kocha wa Yanga, Zltako Krmpotic, aliwashangaa akisema: “Hakuna tatizo lolote juu ya kuanza vibaya kwenye ligi kwani hali hiyo inaweza kuitokea timu yoyote ile. Tulicheza vizuri sana lakini mwisho tukapata matokeo hayo ambayo ni kawaida sana.   “Cha muhimu zaidi ni kwamba kwenye mechi ijayo tutaongeza umakini kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.” MSIMU: 2011/12 MATOKEO: Yanga 0-1 JKT Ruvu NAFASI: 03POINTI: 49   MSIMU: 2012/13 MATOKEO: Prisons 0-0 Yanga NAFASI: 01POINTI: 60MSIMU: 2013/14 MATOKEO: Yanga 5-1 Ashanti NAFASI: 02POINTI: 56MSIMU: 2014/15 MATOKEO: Mtibwa 2-0 Yanga NAFASI: 01POINTI: 55   MSIMU: 2015/16 MATOKEO: Yanga 2-0 Coastal NAFASI: 01POINTI: 73  MSIMU: 2016/17 MATOKEO: Yanga 3-0 African Lyon NAFASI: 01POINTI: 68  MSIMU: 2017/18 MATOKEO: Yanga 1-1 Lipuli NAFASI: 03POINTI: 52  MSIMU: 2018/19 MATOKEO: Yanga 2-1 Mtibwa NAFASI: 02POINTI: 86  MSIMU: 2019/20 MATOKEO: Yanga 0-1 Ruvu NAFASI: 02POINTI: 72  MSIMU: 2020/21 MATOKEO: Yanga 1-1 PrisonsNAFASI: ???POINTI: ???,

HII ni rekodi mpya ya Yanga ambayo imejirudia baada ya kupita takribani misimu kumi ndani ya Ligi Kuu Bara.

 

Yanga ambayo ilianzishwa mwaka 1935, ndiyo mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara baada ya kulitwaa mara 27, wakifuatiwa na Simba wenye mataji 21.

 

Wikiendi iliyopita ambapo Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ilianza, ndiyo Yanga iliweka rekodi hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Prisons kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Rekodi ambayo Yanga imeiweka ni ya kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi ya kwanza ya ligi kwa msimu wa pili mfululizo. Awali iliwahi kufanya hivyo katika msimu wa 2011/12 na 2012/13. Kisha haijawahi kujirudia hadi msimu huu.

 


Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita, Yanga ilianza kwa kupokea kichapo kutoka kwa Ruvu Shooting cha bao 1-0, msimu huu ikatoka sare ya 1-1 na Priosons.

 

Katika msimu wa 2011/12, Yanga ikiwa nyumbani, ilianza ligi kwa kufungwa Yanga 0-1 JKT Ruvu ambayo kwa sasa ni JKT Tanzania, kisha 2012/13 ikatoka 0-0 na Prisons ugenini.

 

Msimu wa 2019/20, Yanga ilifungwa na Ruvu Shooting bao 1-0, kisha msimu huu ikatoka sare ya 1-1 na Prisons. Mechi hizo zote Yanga ilikuwa nyumbani.

 

Wakati Yanga ikianza msimu wa 2011/12 kwa kipigo, ilimaliza ligi nafasi ya tatu ikikusanya pointi 49. Mabingwa walikuwa Simba waliokusanya pointi 62, nafasi ya pili ilishikwa na Azam iliyokuwa na pointi 56.

 

Msimu wa 2012/13, Yanga licha ya kuanza kwa sare, lakini ilikuwa bingwa kwa kukusanya pointi 60. Nafasi ya pili ilishikwa na Azam iliyokuwa na pointi 54 na Simba ya tatu ikiwa na pointi 45.

 

2019/20, Yanga ilipofungwa mechi ya kwanza, ilimaliza ligi nafasi ya pili ikiwa na pointi 72 katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Simba waliokusanya pointi 88.

 

Msimu huu imeanza kwa sare, kitakachotokea mwisho wa msimu kila mmoja anakisubiri kama kitajirudia kile kilichotokea msimu wa 2012/13.

 

Ukiangalia katika rekodi hizo, Yanga ilicheza na timu zote za majeshi ambazo ni JKT Tanzania, Ruvu Shooting na Prisons mara mbili.

 

KOCHA ZLATKO ASHANGAA

Baada ya kuanza ligi kwa sare, mashabiki wa timu hiyo walianza kutoa maneno mengi juu ya kikosi chao hicho ambapo Kocha wa Yanga, Zltako Krmpotic, aliwashangaa akisema: “Hakuna tatizo lolote juu ya kuanza vibaya kwenye ligi kwani hali hiyo inaweza kuitokea timu yoyote ile. Tulicheza vizuri sana lakini mwisho tukapata matokeo hayo ambayo ni kawaida sana.

 

“Cha muhimu zaidi ni kwamba kwenye mechi ijayo tutaongeza umakini kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.”


MSIMU: 2011/12

MATOKEO: Yanga 0-1 JKT Ruvu

NAFASI: 03

POINTI: 49

 

MSIMU: 2012/13

MATOKEO: Prisons 0-0 Yanga

NAFASI: 01

POINTI: 60


MSIMU: 2013/14

MATOKEO: Yanga 5-1 Ashanti

NAFASI: 02

POINTI: 56


MSIMU: 2014/15

MATOKEO: Mtibwa 2-0 Yanga

NAFASI: 01

POINTI: 55

 

MSIMU: 2015/16

MATOKEO: Yanga 2-0 Coastal

NAFASI: 01

POINTI: 73

 

MSIMU: 2016/17

MATOKEO: Yanga 3-0 African Lyon

NAFASI: 01

POINTI: 68

 

MSIMU: 2017/18

MATOKEO: Yanga 1-1 Lipuli

NAFASI: 03

POINTI: 52

 

MSIMU: 2018/19

MATOKEO: Yanga 2-1 Mtibwa

NAFASI: 02

POINTI: 86

 

MSIMU: 2019/20

MATOKEO: Yanga 0-1 Ruvu

NAFASI: 02

POINTI: 72

 

MSIMU: 2020/21

MATOKEO: Yanga 1-1 Prisons

NAFASI: ???

POINTI: ???

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *