Posted By Posted On

AZAM FC YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA COASTAL UNION, DUBE ATAKATA

 PRINCE Dube, mshambuliaji mpya ndani ya Klabu ya Azam FC leo ametimiza majukumu yake kwa kuifungia timu hiyo mabao ya ushindi 2-0 mbele ya Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.Mchezo wa leo, Septemba 11 ulikuwa ni wa kasi na ushindani mkubwa ambapo kipindi cha kwanza mlinda mlango wa Coastal Union, Abubakari Abasi alikuwa nyota wa mchezo kwa kuokoa michomo hatari ya Obrey Chirwa na Prince ambapo walikwenda mapumziko wakiwa wametoshana nguvu ya bila kufungana.Mambo yalibadilika kwa Coastal Union kipindi cha pili  dakika ya 69 ambapo Prince alipachika bao kwanza na dakika ya 89 alipachika bao la pili likiwa ndio bao la usiku mpaka sasa kuliko yote kwa msimu mpya wa 2020/21.Azam FC inakusanya jumla ya pointi sita Uwanja wa Azam Complex ikiwa imefunga jumla ya mabao matatu ambapo mchezo wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania ilishinda kwa bao 1-0 na leo imeshinda mabao 2-0.Coastal Union wao wanayeyusha pointi sita kwa mpigo na kufungwa mabao matatu ambapo mchezo wa kwanza Uwanja wa Majaliwa walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Namungo na leo wamepoteza kwa kufungwa mabao 20 mbele ya Azam FC.,


 PRINCE Dube, mshambuliaji mpya ndani ya Klabu ya Azam FC leo ametimiza majukumu yake kwa kuifungia timu hiyo mabao ya ushindi 2-0 mbele ya Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Mchezo wa leo, Septemba 11 ulikuwa ni wa kasi na ushindani mkubwa ambapo kipindi cha kwanza mlinda mlango wa Coastal Union, Abubakari Abasi alikuwa nyota wa mchezo kwa kuokoa michomo hatari ya Obrey Chirwa na Prince ambapo walikwenda mapumziko wakiwa wametoshana nguvu ya bila kufungana.


Mambo yalibadilika kwa Coastal Union kipindi cha pili  dakika ya 69 ambapo Prince alipachika bao kwanza na dakika ya 89 alipachika bao la pili likiwa ndio bao la usiku mpaka sasa kuliko yote kwa msimu mpya wa 2020/21.


Azam FC inakusanya jumla ya pointi sita Uwanja wa Azam Complex ikiwa imefunga jumla ya mabao matatu ambapo mchezo wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania ilishinda kwa bao 1-0 na leo imeshinda mabao 2-0.


Coastal Union wao wanayeyusha pointi sita kwa mpigo na kufungwa mabao matatu ambapo mchezo wa kwanza Uwanja wa Majaliwa walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Namungo na leo wamepoteza kwa kufungwa mabao 20 mbele ya Azam FC.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *