Posted By Posted On

CHELSEA WAIPOTEZA INTER MILAN KWA KANTE

MABOSI wa Chelsea wameifungia vioo Klabu ya Inter Milan ambayo ilikuwa inahitaji kupata saini ya kiungo N’Golo Kante ili ajiunge na klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.Pia Inter Milan ilikuwa na mpango wa kufanya mabadilishano na wachezaji wawili ambao ni Christian Eriksen na Marcelo Brozovic ili kuwashawishi mabosi wa Chelsea kumuachia Kante.Kante ambaye ni kiungo mwenye miaka 28 amekuwa kwenye ubora wake akiwa ndani ya uwanja ambapo kwa msimu wa 2019/20 alicheza jumla ya mechi 22 ndani ya Ligi Kuu England huku akitupia mabao 3 jambo ambalo limewavutia Inter Milan huku wakiwa hawajakubali uwezo wa Eriksen ndani ya timu yao.Chelsea ipo tayari kumuuza Jorginho kwa sasa na sio Kante ambaye ni raia wa Ufaransa na hawana mpango wa kuwachukua nyota wawili ambao wameambiwa watapewa ikiwa ni pamoja na Eriksen na Brozovic.Nyota wa zamani wa Tottenham, kiungo Eriksen ameshindwa kuonyesha makeke yake ndani ya Inter Milan jambo ambalo linawafanya mabosi hao kufikiria kumuweka sokoni.,


MABOSI wa Chelsea wameifungia vioo Klabu ya Inter Milan ambayo ilikuwa inahitaji kupata saini ya kiungo N’Golo Kante ili ajiunge na klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

Pia Inter Milan ilikuwa na mpango wa kufanya mabadilishano na wachezaji wawili ambao ni Christian Eriksen na Marcelo Brozovic ili kuwashawishi mabosi wa Chelsea kumuachia Kante.

Kante ambaye ni kiungo mwenye miaka 28 amekuwa kwenye ubora wake akiwa ndani ya uwanja ambapo kwa msimu wa 2019/20 alicheza jumla ya mechi 22 ndani ya Ligi Kuu England huku akitupia mabao 3 jambo ambalo limewavutia Inter Milan huku wakiwa hawajakubali uwezo wa Eriksen ndani ya timu yao.

Chelsea ipo tayari kumuuza Jorginho kwa sasa na sio Kante ambaye ni raia wa Ufaransa na hawana mpango wa kuwachukua nyota wawili ambao wameambiwa watapewa ikiwa ni pamoja na Eriksen na Brozovic.

Nyota wa zamani wa Tottenham, kiungo Eriksen ameshindwa kuonyesha makeke yake ndani ya Inter Milan jambo ambalo linawafanya mabosi hao kufikiria kumuweka sokoni.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *