Posted By Posted On

SIMBA KUFANYA MABADILIKO HAYA MAWILI

 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa atafanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi cha kesho kitakachovaana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri ama aina ya uchezaji.Sven amesema kuna mambo mawili ambayo atayafanyia mabadiliko kesho ikiwa itakuwa ni namna ya uchezaji ama wachezaji. Raia huyo wa Ubelgiji amesema:-“Kila mmoja yupo tayari kwa mchezo. Kwangu ni muhimu kuanza vizuri katika michezo ya mwanzoni ili kuwa juu kwenye msimamo kabla ya kwenda kucheza CAFCL,(Ligi ya Mabingwa Afrika).“Mabadiliko yatakuwepo kama sio ya nafasi labda kwenye namna ya uchezaji lakini bado sijaamua.”Simba inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Ihefu huku Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo.Mchezo wao walipokutana ndani ya Uwanja wa Jamhuri msimu wa 2019/20 Simba ilishinda mabao 3-0.,

 

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa atafanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi cha kesho kitakachovaana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri ama aina ya uchezaji.

Sven amesema kuna mambo mawili ambayo atayafanyia mabadiliko kesho ikiwa itakuwa ni namna ya uchezaji ama wachezaji. 

Raia huyo wa Ubelgiji amesema:-“Kila mmoja yupo tayari kwa mchezo. Kwangu ni muhimu kuanza vizuri katika michezo ya mwanzoni ili kuwa juu kwenye msimamo kabla ya kwenda kucheza CAFCL,(Ligi ya Mabingwa Afrika).

“Mabadiliko yatakuwepo kama sio ya nafasi labda kwenye namna ya uchezaji lakini bado sijaamua.”

Simba inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Ihefu huku Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo.

Mchezo wao walipokutana ndani ya Uwanja wa Jamhuri msimu wa 2019/20 Simba ilishinda mabao 3-0.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *