Posted By Posted On

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR

 UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 12, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Tayari kikosi cha Simba kimeshatia timu ndani ya Moro na jana Septemba 10 walianza mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti kumenyana na wapinzani wao.Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanahitaji pointi tatu muhimu.Simba inakutana na Mtibwa Sugar iliyotoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting mchezo wa kwanza Uwanja wa Gairo Moro, huku wao wakishinda kwa mabao 2-1 mbele ya Ihefu,Uwanja wa Sokoine, Mbeya.Msimu uliopita walipokutana Uwanja wa Jamhuri,  Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru Simba ilishinda mabao 2-1.,

 

UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 12, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

Tayari kikosi cha Simba kimeshatia timu ndani ya Moro na jana Septemba 10 walianza mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti kumenyana na wapinzani wao.

Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanahitaji pointi tatu muhimu.

Simba inakutana na Mtibwa Sugar iliyotoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting mchezo wa kwanza Uwanja wa Gairo Moro, huku wao wakishinda kwa mabao 2-1 mbele ya Ihefu,Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Msimu uliopita walipokutana Uwanja wa Jamhuri,  Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru Simba ilishinda mabao 2-1.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *