Posted By Posted On

SIMBA;MCHEZO WETU DHIDI YA MTIBWA SUGAR SIO MWEPESI

 KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo Septemba 12 kitakuwa kazini kumenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri. Mchezo wa leo ni wa pili kwa Simba na Mtibwa Sugar ndani ya msimu mpya wa 2020/21.Katika mchezo uliopita wa ligi, Simba ilifanikiwa kuvuna pointi tatu kwa kuwafunga Ihefu FC mabao 2-1 huku Mtibwa yenyewe ikitoka suluhu na Ruvu Shooting.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ushindani na wanatambua kwamba wanakutana na timu ngumu na yenye ushindani hivyo hautakuwa mchezo mwepesi. Manara amesema kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa na mchezaji ambaye atakosekana kwenye mchezo wa leo hivyo hawana mashaka na suala la wachezaji ni suala la muda kutimiza majukumu pamoja na benchi la ufundi.Miongoni mwa wachezaji ambao walikosekana kwenye mchezo dhidi ya Ihefu likuwa ni pamoja na Luis Miquissone, Gerson Fraga, Chris Mugalu, na Pascal Wawa walioachwa kwenye safari ya Mbeya timu hiyo ilipokwenda kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi na Ihefu FC kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.”Mtibwa sio timu nyepesi na mechi zetu dhidi yao huwa zinakuwa ngumu hilo lipo wazi, kwa sasa wachezaji wote wapo vizuri na wataingia uwanjani wakiwa na nidhamu na kazi yao ni kusaka ushindi ili kufikia malengo yetu.”Mashabiki watupe sapoti na wajitokeze kwa wingi ili tuedelee pale ambapo tuliishia kwenye mchezo wetu dhidi ya Ihefu kwa kupata pointi tatu ili turejee kwenye nafasi yetu,” amesema. Uwanja wa Jamhuri, Morogoro msimu wa 2019/20 Simba ilisepa na pointi tatu kwa ushindi wa mabao 3-0 hivyo leo ni mchezo wa kisasi.,


 KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo Septemba 12 kitakuwa kazini kumenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri.

 

Mchezo wa leo ni wa pili kwa Simba na Mtibwa Sugar ndani ya msimu mpya wa 2020/21.Katika mchezo uliopita wa ligi, Simba ilifanikiwa kuvuna pointi tatu kwa kuwafunga Ihefu FC mabao 2-1 huku Mtibwa yenyewe ikitoka suluhu na Ruvu Shooting.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ushindani na wanatambua kwamba wanakutana na timu ngumu na yenye ushindani hivyo hautakuwa mchezo mwepesi.

 

Manara amesema kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa na mchezaji ambaye atakosekana kwenye mchezo wa leo hivyo hawana mashaka na suala la wachezaji ni suala la muda kutimiza majukumu pamoja na benchi la ufundi.


Miongoni mwa wachezaji ambao walikosekana kwenye mchezo dhidi ya Ihefu likuwa ni pamoja na Luis Miquissone, Gerson Fraga, Chris Mugalu, na Pascal Wawa walioachwa kwenye safari ya Mbeya timu hiyo ilipokwenda kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi na Ihefu FC kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


“Mtibwa sio timu nyepesi na mechi zetu dhidi yao huwa zinakuwa ngumu hilo lipo wazi, kwa sasa wachezaji wote wapo vizuri na wataingia uwanjani wakiwa na nidhamu na kazi yao ni kusaka ushindi ili kufikia malengo yetu.


“Mashabiki watupe sapoti na wajitokeze kwa wingi ili tuedelee pale ambapo tuliishia kwenye mchezo wetu dhidi ya Ihefu kwa kupata pointi tatu ili turejee kwenye nafasi yetu,” amesema.


 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro msimu wa 2019/20 Simba ilisepa na pointi tatu kwa ushindi wa mabao 3-0 hivyo leo ni mchezo wa kisasi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *