Posted By Posted On

ISHU YA JEZI, YANGA YAIPIGA DONGO KIMTINDO SIMBA

 MSHAURI wa Yanga, Senzo Mazingiza raia wa Afrika Kusini, ameibuka na kusema kuwa utengenezaji wa jezi za timu hiyo umetumia ubunifu wa kiwango cha juu huku akifafanua uamuzi wa kuweka ramani ya Afrika kwenye jezi hizo.Senzo ametoa kauli hiyo kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram, baada ya Ijumaa, Septemba 11 Yanga kuzindua jezi zao mpya za msimu huu wa 2020/21.Bosi huyo wa zamani wa Simba, katika ufafanuzi wake huo, ameonekana kama amewatupia dongo kimtindo Simba ambao baada ya kuzinduliwa kwa jezi hizo, mashabiki wanaodaiwa kuwa wa timu hiyo, walianza kuzikejeli.Senzo aliandika: “Ubunifu wa jezi mpya unaonesha vitu. Matarajio ya muundo wa jezi ni kuwapa wachezaji hisia ya kujivunia na kuongeza ujasiri wao, wakijua kuwa vitu vyote vya kiufundi vya teknolojia ya kisasa katika utoaji jasho.“Ubunifu muhimu zaidi pia umejikita katika ramani ya Afrika ambayo pia ni kitu muhimu katika nembo ya klabu, vitu hivi vinahusisha timu na mashabiki wake ambao watavaa jezi hizi kwa kujivunia wakati wanaendelea kuisaidia Yanga.”Wakati huohuo, taarifa zinasema kwamba, mauzo ya jezi hizo yamevunja rekodi ambapo siku ya kwanza tu kuanza kuuzwa, ziliisha zote huku mzigo mpya ukitarajiwa kupatikana kuanzia leo. Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema: “Jezi zimeisha, kesho Jumapili mzigo utaingia kwa ndege kutoka Ethiopia, zitaanza kuuzwa hapa klabuni. Baada ya hapo, wiki ijayo utaingia mzigo mwingine mkubwa ambao jezi hizo zitatosha kusambazwa nchi nzima.”,

 


MSHAURI wa Yanga, Senzo Mazingiza raia wa Afrika Kusini, ameibuka na kusema kuwa utengenezaji wa jezi za timu hiyo umetumia ubunifu wa kiwango cha juu huku akifafanua uamuzi wa kuweka ramani ya Afrika kwenye jezi hizo.

Senzo ametoa kauli hiyo kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram, baada ya Ijumaa, Septemba 11 Yanga kuzindua jezi zao mpya za msimu huu wa 2020/21.


Bosi huyo wa zamani wa Simba, katika ufafanuzi wake huo, ameonekana kama amewatupia dongo kimtindo Simba ambao baada ya kuzinduliwa kwa jezi hizo, mashabiki wanaodaiwa kuwa wa timu hiyo, walianza kuzikejeli.Senzo aliandika: “Ubunifu wa jezi mpya unaonesha vitu.

 

Matarajio ya muundo wa jezi ni kuwapa wachezaji hisia ya kujivunia na kuongeza ujasiri wao, wakijua kuwa vitu vyote vya kiufundi vya teknolojia ya kisasa katika utoaji jasho.


“Ubunifu muhimu zaidi pia umejikita katika ramani ya Afrika ambayo pia ni kitu muhimu katika nembo ya klabu, vitu hivi vinahusisha timu na mashabiki wake ambao watavaa jezi hizi kwa kujivunia wakati wanaendelea kuisaidia Yanga.”


Wakati huohuo, taarifa zinasema kwamba, mauzo ya jezi hizo yamevunja rekodi ambapo siku ya kwanza tu kuanza kuuzwa, ziliisha zote huku mzigo mpya ukitarajiwa kupatikana kuanzia leo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema: “Jezi zimeisha, kesho Jumapili mzigo utaingia kwa ndege kutoka Ethiopia, zitaanza kuuzwa hapa klabuni. Baada ya hapo, wiki ijayo utaingia mzigo mwingine mkubwa ambao jezi hizo zitatosha kusambazwa nchi nzima.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *