Posted By Posted On

KOCHA SIMBA: WACHEZAJI YANGA WAPEWE NAFASI

 KOCHA wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefichua kuwa kwa jinsi kikosi cha Yanga kilivyo msimu huu itachukua muda kuwafikia wapinzani wao Simba. Julio amesema: “Ukiangalia Simba tayari wameshakaa muda mrefu wakiwa pamoja na hata ukiangalia walivyocheza kwenye Ngao ya Jamii tayari walikuwa wakicheza kitimu tofauti na Yanga ambao bado wanajenga timu yao kutokana na wachezaji wengi kuwa wapya.“Ukweli itawachukua muda kukaa sawa ili kuweza kwenda na kasi ya ligi lakini Yanga pia kocha anatakiwa kuwa makini katika ubadilishaji na upangaji wa kikosi.”Mchezaji kama Kaseke,(Deus) anatakiwa kucheza ila sio muda mrefu na kiungo mpya yule Farid Mussa anaonyesha ana kitu hivyo ni suala la kusubiri na kuona nini kitatokea kwao ila wanapaswa kuwa na subira.”Yanga jana ilishinda kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City na kuvunja rekodi ya msimu uliopita kwa kushindwa kuvuna pointi tatu kwenye mechi zote mbili.Bao pekee la Yanga lilipachikwa kimiani na beki kisiki, Lamine Moro kwa kichwa ndani ya 18 akimalizia kazi ya kona iliyochongwa na Muangola, Carlos Carlinhos ambaye aliingia uwanjani dakika ya 60 akichukua nafasi ya Feisal Salum.,


 KOCHA wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefichua kuwa kwa jinsi kikosi cha Yanga kilivyo msimu huu itachukua muda kuwafikia wapinzani wao Simba.

 

Julio amesema: “Ukiangalia Simba tayari wameshakaa muda mrefu wakiwa pamoja na hata ukiangalia walivyocheza kwenye Ngao ya Jamii tayari walikuwa wakicheza kitimu tofauti na Yanga ambao bado wanajenga timu yao kutokana na wachezaji wengi kuwa wapya.


“Ukweli itawachukua muda kukaa sawa ili kuweza kwenda na kasi ya ligi lakini Yanga pia kocha anatakiwa kuwa makini katika ubadilishaji na upangaji wa kikosi.


“Mchezaji kama Kaseke,(Deus) anatakiwa kucheza ila sio muda mrefu na kiungo mpya yule Farid Mussa anaonyesha ana kitu hivyo ni suala la kusubiri na kuona nini kitatokea kwao ila wanapaswa kuwa na subira.”


Yanga jana ilishinda kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City na kuvunja rekodi ya msimu uliopita kwa kushindwa kuvuna pointi tatu kwenye mechi zote mbili.


Bao pekee la Yanga lilipachikwa kimiani na beki kisiki, Lamine Moro kwa kichwa ndani ya 18 akimalizia kazi ya kona iliyochongwa na Muangola, Carlos Carlinhos ambaye aliingia uwanjani dakika ya 60 akichukua nafasi ya Feisal Salum.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *