Posted By Posted On

SVEN ATAJA KINACHOISUMBUA TIMU YAKE KWA SASA

JANA  Jumamosi, Septemba 12, Simba ilibanwa mbavu na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amemtaja mchawi ambaye anaweza kuwazuia wasiwe mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Simba ikiwa na kikosi chake kamili, ililazimishwa sare ya bao 1-1 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mzamiru Yassin alikuwa wa kwanza kuitanguliza Simba mbele kwa bao lake dakika ya 45 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Mtibwa Sugar.Mapema tu kipindi cha pili dakika ya 46, Boban Zirintusa aliisawazishia Mtibwa na kufanya matokeo kuwa 1-1. Licha ya timu zote kufanya mabadiliko ya mara kwa mara, lakini hakuna timu iliyoongeza bao, hadi mwisho matokeo yakawa 1-1.Sven msimu huu ana kazi ya kutetea ubingwa wa ligi hiyo, amesema: “Licha ya usajili bora ambao kikosi chetu kimeufanya, lakini kuna changamoto moja ambayo inaweza kutuzuia tusiwe mabingwa.“Changamoto kubwa ambayo ninaiona tutakuwa nayo msimu huu ni ile ya kutafuta uwiano kwenye maeneo mawili ambayo ni eneo la ushambuliaji na ulinzi, naamini kama tutaweza kutengeneza muunganiko mzuri katika maeneo hayo basi naamini hakuna wa kutuzuia kutwaa ubingwa,” alisema Sven. Matokeo mengine ya mechi za jana ni; JKT Tanzania 0-2 Dodoma Jiji, mabao ya Dodoma yalifungwa na Jamal Mtegeta dakika ya 50 na Dickson Ambundo (dk 80). KMC 2-1 Prisons, wafungaji wa KMC ni Hassan Kabunda dakika ya 21 na Keneth Masumbuko (dk 90), lile la Prisons lilifungwa na Kassim Mdoe dakika ya 39.,


JANA  Jumamosi, Septemba 12, Simba ilibanwa mbavu na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amemtaja mchawi ambaye anaweza kuwazuia wasiwe mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.


Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Simba ikiwa na kikosi chake kamili, ililazimishwa sare ya bao 1-1 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Mzamiru Yassin alikuwa wa kwanza kuitanguliza Simba mbele kwa bao lake dakika ya 45 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Mtibwa Sugar.Mapema tu kipindi cha pili dakika ya 46, Boban Zirintusa aliisawazishia Mtibwa na kufanya matokeo kuwa 1-1.

 

Licha ya timu zote kufanya mabadiliko ya mara kwa mara, lakini hakuna timu iliyoongeza bao, hadi mwisho matokeo yakawa 1-1.


Sven msimu huu ana kazi ya kutetea ubingwa wa ligi hiyo, amesema: “Licha ya usajili bora ambao kikosi chetu kimeufanya, lakini kuna changamoto moja ambayo inaweza kutuzuia tusiwe mabingwa.


“Changamoto kubwa ambayo ninaiona tutakuwa nayo msimu huu ni ile ya kutafuta uwiano kwenye maeneo mawili ambayo ni eneo la ushambuliaji na ulinzi, naamini kama tutaweza kutengeneza muunganiko mzuri katika maeneo hayo basi naamini hakuna wa kutuzuia kutwaa ubingwa,” alisema Sven.

 

Matokeo mengine ya mechi za jana ni; JKT Tanzania 0-2 Dodoma Jiji, mabao ya Dodoma yalifungwa na Jamal Mtegeta dakika ya 50 na Dickson Ambundo (dk 80). KMC 2-1 Prisons, wafungaji wa KMC ni Hassan Kabunda dakika ya 21 na Keneth Masumbuko (dk 90), lile la Prisons lilifungwa na Kassim Mdoe dakika ya 39.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *