Posted By Posted On

YANGA V MBEYA CITY LEO KWA MKAPA KUSAKA POINTI TATU

KWA Msimu wa 2019/20 mechi zote mbili kati ya Yanga v Mbeya City hakuna mbabe aliyesepa na pointi tatu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.Mchezo wa kwanza, Mbeya City ilizimisha sare ya bila kufungana Uwanja wa Sokoine kisha mchezo wa pili, Uwanja wa Mkapa zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.Kwenye pointi sita ambazo walikuwa wanasaka msimu uliopita wote wawili waligawana pointi mbilimbili na kuziyeyusha pointi nne jumlajumla.Leo Septemba 13 zinakutana Uwanja wa Mkapa,mchezo unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku.Kocha Mkuu wa Mbeya City, Amri Said  amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.Mechi zao za ligi  zilizopita msimu mpya wa 2020/21, Mbeya City ilichapwa mabao 4-0 mbele ya KMC, Uwanja wa Uhuru na Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.Yanga itaingia uwanjani kwa hali ya kujiamini na kusaka ushindi ili kuwapoteza wapinzani wao Simba ambao jana walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.,

KWA Msimu wa 2019/20 mechi zote mbili kati ya Yanga v Mbeya City hakuna mbabe aliyesepa na pointi tatu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.


Mchezo wa kwanza, Mbeya City ilizimisha sare ya bila kufungana Uwanja wa Sokoine kisha mchezo wa pili, Uwanja wa Mkapa zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.


Kwenye pointi sita ambazo walikuwa wanasaka msimu uliopita wote wawili waligawana pointi mbilimbili na kuziyeyusha pointi nne jumlajumla.


Leo Septemba 13 zinakutana Uwanja wa Mkapa,mchezo unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku.


Kocha Mkuu wa Mbeya City, Amri Said  amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Mechi zao za ligi  zilizopita msimu mpya wa 2020/21, Mbeya City ilichapwa mabao 4-0 mbele ya KMC, Uwanja wa Uhuru na Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.


Yanga itaingia uwanjani kwa hali ya kujiamini na kusaka ushindi ili kuwapoteza wapinzani wao Simba ambao jana walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *