Posted By Posted On

HESABU ZA SIMBA KWA SASA ZIPO KWA BIASHARA UNITED

 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa akili zote wanazielekeza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa.Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Septemba 12.Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kutwaa ubingwa hivyo wanachofikiria ni ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Biashara.“Malengo yetu makubwa ni kuona kwamba tunaweza kushinda mechi yetu ijayo, kupata sare kwenye mchezo wetu uliopita unaweza kusema kuwa sio matokeo mazuri lakini hakuna namna kwa kuwa tumecheza kwenye mazingira magumu hasa sehemu ya kuchezea.“Mchezo wetu unaofuata ndio tunautazama kwa ukaribu na tunahitaji kupata pointi tatu kwa kuwa tunahitaji kutwaa tena taji la ligi ambalo lipo mikononi mwetu,” amesema Manara. Simba kibindoni ina pointi nne ndani ya mechi mbili ambazo wamecheza na imetupia mabao matatu huku ikiokota nyavuni mabao mawili.,

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa akili zote wanazielekeza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Septemba 20, Uwanja wa Mkapa.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Septemba 12.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kutwaa ubingwa hivyo wanachofikiria ni ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Biashara.

“Malengo yetu makubwa ni kuona kwamba tunaweza kushinda mechi yetu ijayo, kupata sare kwenye mchezo wetu uliopita unaweza kusema kuwa sio matokeo mazuri lakini hakuna namna kwa kuwa tumecheza kwenye mazingira magumu hasa sehemu ya kuchezea.

“Mchezo wetu unaofuata ndio tunautazama kwa ukaribu na tunahitaji kupata pointi tatu kwa kuwa tunahitaji kutwaa tena taji la ligi ambalo lipo mikononi mwetu,” amesema Manara.

 Simba kibindoni ina pointi nne ndani ya mechi mbili ambazo wamecheza na imetupia mabao matatu huku ikiokota nyavuni mabao mawili.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *