Posted By Posted On

IDD CHECHE APANIA KUREJEA NDANI YA LIGI KUU BARA

 KOCHA Mkuu wa Kitayosce FC, Idd Cheche ambaye aliwahi kuifundisha pia Azam FC amesema kuwa atahakikisha timu hiyo inafanya vyema katika michezo yake ili iweze kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao.Cheche alisimamishwa ndani ya Azam FC msimu wa 2019/20 nafasi yake kwenye benchi la ufundi la kikosi hicho ambacho kwa sasa kinanolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, raia wa Romania. Cheche amesema kuwa:- “Napenda kuwashukuru viongozi wa Kitayosce ya hapa Tabora kwa kuniamini kufanya kazi na mimi, naamini nimekuja sehemu sahihi ambayo itanifanya nipambane mpaka mwisho katika kuhakikisha timu hii inafanya vizuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza.“Kikubwa ninachowaomba wakazi wa Tabora ni ushirikiano kwa kazi ambayo nimekuja kufanya hapa na kwa kuwa mkoa huu umekosa timu kwa zaidi ya miaka saba mpaka sasa tutapambana ili kupanda ligi,” amesema.  Kitayosce  imepanda daraja kutoka Ligi Daraja la Pili na itacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu huu. Imesajili wachezaji wakongwe miongoni mwao ni Hussein Javu na Jamal Mnyate na wengine wengi lengo ikiwa ni kuhakikisha kwamba timu hiyo inapanda ligi kuu. ,

 


KOCHA Mkuu wa Kitayosce FC, Idd Cheche ambaye aliwahi kuifundisha pia Azam FC amesema kuwa atahakikisha timu hiyo inafanya vyema katika michezo yake ili iweze kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao.

Cheche alisimamishwa ndani ya Azam FC msimu wa 2019/20 nafasi yake kwenye benchi la ufundi la kikosi hicho ambacho kwa sasa kinanolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, raia wa Romania.

 

Cheche amesema kuwa:- “Napenda kuwashukuru viongozi wa Kitayosce ya hapa Tabora kwa kuniamini kufanya kazi na mimi, naamini nimekuja sehemu sahihi ambayo itanifanya nipambane mpaka mwisho katika kuhakikisha timu hii inafanya vizuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza.

“Kikubwa ninachowaomba wakazi wa Tabora ni ushirikiano kwa kazi ambayo nimekuja kufanya hapa na kwa kuwa mkoa huu umekosa timu kwa zaidi ya miaka saba mpaka sasa tutapambana ili kupanda ligi,” amesema.

 

 

Kitayosce  imepanda daraja kutoka Ligi Daraja la Pili na itacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu huu. Imesajili wachezaji wakongwe miongoni mwao ni Hussein Javu na Jamal Mnyate na wengine wengi lengo ikiwa ni kuhakikisha kwamba timu hiyo inapanda ligi kuu.

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *