Posted By Posted On

Ihefu yazinduka, Biashara yaendeleza ubabe VPL

NA ZAINAB IDDY TIMU ya Ihefu FC imezinduka baada ya kushinda mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ikitoka kupokea kipigo cha mabao 201 kutoka kwa Simba katika mchezo wa kwanza. Ihefu ambayo imepanda daraja msimu huu, jana ilipata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting katika mechi yao hiyo ya pili,

NA ZAINAB IDDY

TIMU ya Ihefu FC imezinduka baada ya kushinda mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ikitoka kupokea kipigo cha mabao 201 kutoka kwa Simba katika mchezo wa kwanza.

Ihefu ambayo imepanda daraja msimu huu, jana ilipata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting katika mechi yao hiyo ya pili kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Katika mchezo wa jana, bao la Ihefu lililodumu kwa dakika 80, lilipatikana kupitia kwa Enoclk Jiah dakika ya saba, aliyepiga shuti la kawaida wakati kipa wa Ruvu Shooting akiwa hayupo katika eneo lake.

Ushindi huo wa Ihefa, umewapandisha hadi nafasi ya saba kutoka ile ya 12 waliyokuwa awali, kwa sasa wakiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi mbili.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Karume, mkoani Mara, wenyeji Biashara United, wameendeleza ushindi kwa kuifunga Mwadui FC bao 1-0, shujaa wao akiwa ni Deogratius Judik aliyecheka na nyavu dakika ya 72.

Katika mchezo wao wa kwanza wiki iliyopita, Biashara iliichapa Gwambina FC bao 1-0 kwenye uwanja huo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *