Posted By Posted On

Katwila afichua siri nzito sare mfululizo

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila, ametaja sababu ya kupata sare katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba ni wachezaji wengi ni wageni katika kikosi chake. Mtibwa Sugar walipata sare  ya bao 1-1 na Simba katika mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Kabla ya matokeo,

NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila, ametaja sababu ya kupata sare katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba ni wachezaji wengi ni wageni katika kikosi chake.

Mtibwa Sugar walipata sare  ya bao 1-1 na Simba katika mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Kabla ya matokeo hayo, Mtibwa Sugar walitoka suluhu na Ruvu Shooting katika mchezo wa kwanza uliochezwa Septemba 7, nmwaka huu,kwenye Uwanja wa Gairo, mkoani humo.

Akizungumza na BINGWA jana, Katwila alisema msimu huu ana wachezaji nane wapya ambao lazima awatumie ili kupata muunganiko anaouhitaji.

“Nimesajili wachezaji nane msimu huu, wote nimekuwa nikiwatumia katika kila mchezo, jambo ambalo linaleta shida kupata matokeo ya ushindi kwa haraka.

“Lengo la kuwatumia wachezaji wote wageni kwa pamoja ni kupata kombinesheni nzuri, hadi raundi ya tano bila shaka watakuwa wameelewana,” alisema Katwila.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *