Posted By Posted On

Kisu atamani namba Stars

NA ZAINAB IDDY KIPA wa Azam, David Kisu, amesema kuwa ndoto yake ni kupata nafasi ya kudaka katika kikosi cha kwanza cha timu ya Taifa, Taifa Stars. Kisu amejiunga na Azam msimu huu wa Ligi Tanzania Bara kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea Klabu ya Gor Mahia inayoshiriki Ligi Kuu Kenya. Tangu ajiunge na Klabu,

NA ZAINAB IDDY

KIPA wa Azam, David Kisu, amesema kuwa ndoto yake ni kupata nafasi ya kudaka katika kikosi cha kwanza cha timu ya Taifa, Taifa Stars.

Kisu amejiunga na Azam msimu huu wa Ligi Tanzania Bara kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea Klabu ya Gor Mahia inayoshiriki Ligi Kuu Kenya.

Tangu ajiunge na Klabu ya Azam, kipa huyo amedaka michezo tatu, miwili ya Ligi Kuu na mmoja wa kirafiki dhidi ya Namungo, huku kikosi chake kikishinda yote.

Akizungumza na BINGWA jana, Dar es Salaam, Kisu alisema anatamani kuona siku moja anakuwa kipa wa kutegemewa katika kikosicha Taifa Stars.

“Najua kuna upinzani makali kutoka kwa makipa wenzangu ambao wamejitengenezea mazingira mazuri kama Aishi Manula na Metacha Mnata, lakini haitanikatisha tamaa.

“Nitapambana katika timu yangu kuhakikisha napata namba ya kudumu, pia nikiitwa Stars sitakuwa tayari kuona naishia kukaa benchi tu,” alisema Kisu.

Kwa sasa Kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amekuwa wakiita makipa Juma Kaseja, Manula na Mnata katika michuano ya kimataifa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *