Posted By Posted On

KOCHA SIMBA AWABADILISHIA MBINU MORRISON NA ONYANGO

 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa atawabadilishia mbinu wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison na Joash Onyango kwa ajili ya kuwaandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Simba itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.Sven ameliambia Spoti Xtra kuwa mpango mkubwa wa timu ni kuweza kufikia malengo hasa kwenye michuano ya kimataifa kwa kuwa wanahitaji kufika hatua ya makundi.“Kwa sasa tuna mechi za kucheza kwenye ligi kabla ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ntakachokifanya ni kuweza kuangalia namna bora hasa kwa wachezaji wangu kuweza kuwapa muda mzuri wa kujiandaa kwa ajili ya michuano ya kimataifa.“Ipo wazi kwamba tunahitaji ubingwa ila haitawezekana ikiwa hatutakuwa na mipango makini, imani yangu ni kwamba wachezaji wapo tayari na tutafanya makubwa,kikubwa sapoti,” alisema.Kwa sasa Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 20.Mchezo wake wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa msimu uliopita mbele ya Biashara United Simba ilishinda mabao 3-1 hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa. ,

 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa atawabadilishia mbinu wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison na Joash Onyango kwa ajili ya kuwaandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.

Sven ameliambia Spoti Xtra kuwa mpango mkubwa wa timu ni kuweza kufikia malengo hasa kwenye michuano ya kimataifa kwa kuwa wanahitaji kufika hatua ya makundi.

“Kwa sasa tuna mechi za kucheza kwenye ligi kabla ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ntakachokifanya ni kuweza kuangalia namna bora hasa kwa wachezaji wangu kuweza kuwapa muda mzuri wa kujiandaa kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

“Ipo wazi kwamba tunahitaji ubingwa ila haitawezekana ikiwa hatutakuwa na mipango makini, imani yangu ni kwamba wachezaji wapo tayari na tutafanya makubwa,kikubwa sapoti,” alisema.

Kwa sasa Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 20.


Mchezo wake wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa msimu uliopita mbele ya Biashara United Simba ilishinda mabao 3-1 hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa.

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *