Posted By Posted On

LAMINE MORO: TUNAHITAJI KUWA NA MWENDELEZO MZURI

 LAMINE Moro, beki kisiki wa Yanga amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuwa na mwendelezo mzuri katika mechi zao zote ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.Moro alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City, Jana Septemba 13, Uwanja wa Mkapa na alifunga bao la ushindi kwa kichwa dakika ya 86 na kuwanyanyua mashabiki wa timu hiyo ambao walijitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi nne kibindoni baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 ndani ya ligi. Ilianza kumenyana na Tanzania Prisons na ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 kisha ikashinda mbele ya Mbeya City bao 1-0.Beki huyo amesema:”Haikuwa kazi rahisi ila kwa sasa tunaachana na matokeo ya mechi yetu iliyopita kwa sasa tunatazama mechi zetu za mbele ambazo ni muhimu kwetu kushinda na hilo linawezekana.”Kikubwa tunahitaji sapoti kutoka kwa mashabiki ili tuweze kuendelea kuwa bora kwani sapoti yao ni muhimu kwetu.” Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Kagera Sugar inayonolewa na Meck Maxime utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.Itakuwa ni Septemba 19. Walipokutana Uwanja wa Kaitaba msimu wa 2019/20, Yanga ilishinda bao 1-0.,

 


LAMINE Moro, beki kisiki wa Yanga amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuwa na mwendelezo mzuri katika mechi zao zote ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.


Moro alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City, Jana Septemba 13, Uwanja wa Mkapa na alifunga bao la ushindi kwa kichwa dakika ya 86 na kuwanyanyua mashabiki wa timu hiyo ambao walijitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.


Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi nne kibindoni baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 ndani ya ligi. Ilianza kumenyana na Tanzania Prisons na ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 kisha ikashinda mbele ya Mbeya City bao 1-0.


Beki huyo amesema:”Haikuwa kazi rahisi ila kwa sasa tunaachana na matokeo ya mechi yetu iliyopita kwa sasa tunatazama mechi zetu za mbele ambazo ni muhimu kwetu kushinda na hilo linawezekana.

“Kikubwa tunahitaji sapoti kutoka kwa mashabiki ili tuweze kuendelea kuwa bora kwani sapoti yao ni muhimu kwetu.” 


Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Kagera Sugar inayonolewa na Meck Maxime utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.


Itakuwa ni Septemba 19. Walipokutana Uwanja wa Kaitaba msimu wa 2019/20, Yanga ilishinda bao 1-0.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *