Posted By Posted On

NYOTA AZAM FC APATA SHAVU ISRAEL

 NYOTA wa Azam FC, Novatus Dismas mwenye tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa msimu wa 2019/20 alipokuwa akikipiga ndani ya Bashara United kwa mkopo amepata shavu la kwenda kufanya majaribio ndani ya Klabu ya Maccabi Tel Aviv ya Israel.Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Israel ipo chini ya Kocha Mkuu, Grovigos Donis na inatumia Uwanja wa Bloom Field wenye uwezo wa kubeba watazamaji 29,150 msimu wa 2019/20 ilitwaa taji lake la kwanza la ligi.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kiungo huyo kwa sasa hayupo nchini kwa kuwa amekwenda kufanya majaribio na klabu ya Israel atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Sokoine, Septemba 20.“Kwa sasa Novatus Dismas hayupo nchini ameenda Israel kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye Klabu ya Maccabi Tel Aviv na hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza dhidi ya Coastal Union,” amesema.Kwa sasa Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba inajiandaa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Septemba 20, Uwanja wa Sokoine kibindoni ina pointi sita baada ya kucheza mechi mbili.Ilishinda mchezo wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania bao 1-0 kisha ikashinda kwa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na mechi zote zilipigwa Azam Complex.,

 


NYOTA wa Azam FC, Novatus Dismas mwenye tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa msimu wa 2019/20 alipokuwa akikipiga ndani ya Bashara United kwa mkopo amepata shavu la kwenda kufanya majaribio ndani ya Klabu ya Maccabi Tel Aviv ya Israel.

Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Israel ipo chini ya Kocha Mkuu, Grovigos Donis na inatumia Uwanja wa Bloom Field wenye uwezo wa kubeba watazamaji 29,150 msimu wa 2019/20 ilitwaa taji lake la kwanza la ligi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kiungo huyo kwa sasa hayupo nchini kwa kuwa amekwenda kufanya majaribio na klabu ya Israel atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Sokoine, Septemba 20.

“Kwa sasa Novatus Dismas hayupo nchini ameenda Israel kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye Klabu ya Maccabi Tel Aviv na hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza dhidi ya Coastal Union,” amesema.

Kwa sasa Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba inajiandaa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Septemba 20, Uwanja wa Sokoine kibindoni ina pointi sita baada ya kucheza mechi mbili.


Ilishinda mchezo wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania bao 1-0 kisha ikashinda kwa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na mechi zote zilipigwa Azam Complex.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *