Posted By Posted On

OFISA HABARI WA SIMBA NA WA YANGA WAPIGWA FAINI

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewatoza faini ya shilingi milioni tano kila mmoja Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya Shirikisho hilo, Zakaria Hanspope kutokana na makosa mbalimbali ya kimaadili huku wakitakiwa kutotenda kosa lolote la kimaadili ndani ya miaka miwili.Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, Wakili Kichere Mwita Waissaka amesoma leo Septemba 14 uamuzi wa kamati hiyo makao makuu ya TFF mbele ya waandishi wa habari. Kwa upande wa Manara amekutwa na hatia kwa kuingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji wakati wa kesi ya mchezaji Bernard Morrison kwa maneno aliyoyatoa kupitia Wasafi Media.Bumbuli yeye amekutwa na hatia ya kusema uongo kwa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kwamba hawajapeleka nakala ya hukumu ya kamati wakati nakala ilifikishwa kwenye klabu yake siku moja kabla ya yeye kuongea na Wasafi Media.Kwa upande wa Hanspope amekutwa na hatia katika makosa mawili:-  Kutoa taarifa ya muenendo wa shauri ambalo lilikuwa linajadiliwa huku yeye akiwa ni mjumbe wa kamati hiyo na kuchochea umma kuhusu sakata la mchezaji Bernard Morrison.Kamati hiyo imesema rufaa ziko wazi.  ,

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewatoza faini ya shilingi milioni tano kila mmoja Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Mjumbe wa Kamati ya Sheria ya Shirikisho hilo, Zakaria Hanspope kutokana na makosa mbalimbali ya kimaadili huku wakitakiwa kutotenda kosa lolote la kimaadili ndani ya miaka miwili.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, Wakili Kichere Mwita Waissaka amesoma leo Septemba 14 uamuzi wa kamati hiyo makao makuu ya TFF mbele ya waandishi wa habari. 

Kwa upande wa Manara amekutwa na hatia kwa kuingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji wakati wa kesi ya mchezaji Bernard Morrison kwa maneno aliyoyatoa kupitia Wasafi Media.


Bumbuli yeye amekutwa na hatia ya kusema uongo kwa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kwamba hawajapeleka nakala ya hukumu ya kamati wakati nakala ilifikishwa kwenye klabu yake siku moja kabla ya yeye kuongea na Wasafi Media.


Kwa upande wa Hanspope amekutwa na hatia katika makosa mawili:-  Kutoa taarifa ya muenendo wa shauri ambalo lilikuwa linajadiliwa huku yeye akiwa ni mjumbe wa kamati hiyo na kuchochea umma kuhusu sakata la mchezaji Bernard Morrison.


Kamati hiyo imesema rufaa ziko wazi.  

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *