Posted By Posted On

POLISI TANZANIA YAITUNGUA BAO 1-0 NAMUNGO, MAJALIWA

 KIKOSI cha Polisi Tanzania leo Septemba 14 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi mbele ya Namungo FC.Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wa mwisho kukamilisha mzunguko wa pili ndani ya msimu mpya wa 2020/21 ulikuwa na ushindani mkali ambapo iliwachukua Polisi Tanzania dakika 76 kupata bao la ushindi.Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Rashid Juma ambaye  alianza kwa kusugua benchi kuusoma mchezo kablaya kuingia akichukua nafasi ya Pius Buswita, alimtungua mlinda mlango Nurdin Barola akiwa nje ya 18 kwa shuti kali la guu lake la kulia akiwa nje ya 18.Ushindi huo unakuwa wa kwanza kwa Polisi Tanzania msimu mpya wa 2020/21 baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Azam FC, Septemba 7, Uwanja wa Azam Complex huku Namungo nao pia wakionja joto ya kupoteza pointi tatu mapema ndani ya Uwanja wao wa nyumbani wa Majaliwa.Mchezo wa kwanza Namungo FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Coastal Union, Septemba 6, Uwanja wa Majaliwa.,

 


KIKOSI cha Polisi Tanzania leo Septemba 14 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi mbele ya Namungo FC.


Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wa mwisho kukamilisha mzunguko wa pili ndani ya msimu mpya wa 2020/21 ulikuwa na ushindani mkali ambapo iliwachukua Polisi Tanzania dakika 76 kupata bao la ushindi.


Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Rashid Juma ambaye  alianza kwa kusugua benchi kuusoma mchezo kablaya kuingia akichukua nafasi ya Pius Buswita, alimtungua mlinda mlango Nurdin Barola akiwa nje ya 18 kwa shuti kali la guu lake la kulia akiwa nje ya 18.

Ushindi huo unakuwa wa kwanza kwa Polisi Tanzania msimu mpya wa 2020/21 baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Azam FC, Septemba 7, Uwanja wa Azam Complex huku Namungo nao pia wakionja joto ya kupoteza pointi tatu mapema ndani ya Uwanja wao wa nyumbani wa Majaliwa.


Mchezo wa kwanza Namungo FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Coastal Union, Septemba 6, Uwanja wa Majaliwa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *