Posted By Posted On

SIMBA KUANZA KUIWINDA BIASHARA UNITED

 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, kesho kinatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.Simba ilikuwa Morogoro ambapo Septemba 12 ilimenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi na kutoshana nguvu kwa kufugana bao 1-1.Kiliporejea Bongo jana, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja kujiweka sawa na kesho wanatarajiwa kuanza mazoezi rasmi kuiwinda Biashara United. Mchezo huo wa mzunguko wa tatu kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi utapigwa Septemba 20, Jumapili Uwanja wa Mkapa na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu za kushinda mchezo mmoja kati ya miwili iliyocheza msimu huu ambapo ilishinda mbele ya Ihefu na kulazimisha sare moja mbele ya Mtibwa Sugar.Walipokutana na Biashara United inayonolewa na Francis Baraza msimu uliopita Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 3-1 hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wa kisasi kwa Biashara United.,


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, kesho kinatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.

Simba ilikuwa Morogoro ambapo Septemba 12 ilimenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi na kutoshana nguvu kwa kufugana bao 1-1.


Kiliporejea Bongo jana, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja kujiweka sawa na kesho wanatarajiwa kuanza mazoezi rasmi kuiwinda Biashara United. 

Mchezo huo wa mzunguko wa tatu kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi utapigwa Septemba 20, Jumapili Uwanja wa Mkapa na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu za kushinda mchezo mmoja kati ya miwili iliyocheza msimu huu ambapo ilishinda mbele ya Ihefu na kulazimisha sare moja mbele ya Mtibwa Sugar.


Walipokutana na Biashara United inayonolewa na Francis Baraza msimu uliopita Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 3-1 hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wa kisasi kwa Biashara United.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *