Posted By Posted On

Simeone akutwa na Corona

MADRID, Hispania KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone, juzi alishindwa kuungana na kikosi hicho mazoezini na ndipo ilipoelezwa kuwa amegundulika kuwa na virusi vya Corona. Kukosekana kwa Simeone raia wa Argentina kulisababisha kocha wa viungo, Profe Ortega, avae viatu vyake lakini wakati huo haikufahamuika sababu ya bosi wake kutofika mazoezini. Awali, Simeone na kila mfanyakazi,

MADRID, Hispania

KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone, juzi alishindwa kuungana na kikosi hicho mazoezini na ndipo ilipoelezwa kuwa amegundulika kuwa na virusi vya Corona.

Kukosekana kwa Simeone raia wa Argentina kulisababisha kocha wa viungo, Profe Ortega, avae viatu vyake lakini wakati huo haikufahamuika sababu ya bosi wake kutofika mazoezini.

Awali, Simeone na kila mfanyakazi ndani ya klabu hiyo alifanyiwa vipimo, kabla ya madaktari kuja na majibu hayo juzi yakionesha mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 50 ameathirika.

Hata hivyo, bahati kwao ni kwamba Atletico haitacheza mechi ya ushindani hadi Septemba 27, mwaka huu, siku itakaposhuka dimbani kuikabili Granada katika dakika 90 za La Liga.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *