Posted By Posted On

Uwanja wa kisasa Yanga wanukia

NA ZAINAB IDDY YANGA wapo mbioni kumtangaza mzabuni atakayejenga uwanja wa kisasa wa klabu hiyo, baada ya hatua ya pili ya  michoro kukamilika. Kamati ya Ujenzi ya Uwanja wa  Klabu ya Yanga inayoongozwa na Bahari Mwaseba, ilikutana juzi jioni, jijini kwa lengo la kuendelea na mipango ya kufanikisha ujenzi huo, unaotarajiwa kujengwa Kigamboni, Dar es,

NA ZAINAB IDDY

YANGA wapo mbioni kumtangaza mzabuni atakayejenga uwanja wa kisasa wa klabu hiyo, baada ya hatua ya pili ya  michoro kukamilika.

Kamati ya Ujenzi ya Uwanja wa  Klabu ya Yanga inayoongozwa na Bahari Mwaseba, ilikutana juzi jioni, jijini kwa lengo la kuendelea na mipango ya kufanikisha ujenzi huo, unaotarajiwa kujengwa Kigamboni, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Dar es Salaam, Mwaseba alisema katika kikao hicho walikabidhi ripoti na bajeti ya ujenzi huo.

“Tumekamilisha jambo muhimu katika harakati za ujezi wa Uwanja wa Yanga, michoro ipo tayari na gharama za ujenzi wa awamu ya kwanza.

“Hatua inayofuata ni kutangaza ‘tender’ (mzabuni) ili kumpata mkandarasi, tukishampata tutawapelekea ripoti wananchi wenye timu yao ili wajue ni eneo lipi tunahitaji nguvu ya pamoja na mikakati ya ujenzi ipo vipi.

 “Matumaini yetu tutatekeleza mradi huu kwa ushirikiano wa karibu na wadhamini wetu na muda ukifika watasema ni kwa manma gani watashiriki katika hili  kwa sababu huu ni mradi mkubwa wenye viwanja viwili, hosteli, bwawa la kuogelea na huduma nyingine,” alisema Mwaseba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *