Posted By Posted On

AZAM FC :TUNATAKA KUENDELEZA KUPATA USHINDI

 BAADA ya ushindi katika michezo miwili mfululizo waliopata timu ya Azam FC, uongozi wa timu hiyo umetamba kuendeleza ushindi katika michezo inayofuata ya ligi kuu. Azam FC katika michezo miwili iliyocheza ya ligi hiyo, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, kisha wakashinda 2-0 dhidi ya Coastal Union, michezo yote ilifanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi jijini Dar.Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya raundi mbili kukamilika inakwenda kumenyana na Mbeya City ya Mbeya ambayo ipo nafasi ya 18 baada ya kucheza mechi mbili pia. Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, amesema kuwa wao wanashukuru kuanza ligi vizuri kwa kupata pointi zote sita muhimu huku akisema kuwa kilichobaki kwao ni kuendeleza ushindi katika michezo inayofuata. “Tunashukuru tumeanza ligi kwa ushindi katika michezo yetu miwili mfululizo, ni pointi sita muhimu kwetu ambazo tulikuwa tukizihitaji kutokana na malengo ambayo tumejiwekea msimu huu kuwa mabingwa wa ligi kuu. “Kwa sasa baada ya ushindi huu ni kutafuta mwendelezo wa ushindi katika michezo yetu ijayo ili tujiwekee nafasi ya kuokota pointi nyingi mapema, hakuna kitu kinachoshindikana zaidi ya kujituma kwa wachezaji na kufuatisha maelekezo ya mwalimu,” amesema.,

 


BAADA ya ushindi katika michezo miwili mfululizo waliopata timu ya Azam FC, uongozi wa timu hiyo umetamba kuendeleza ushindi katika michezo inayofuata ya ligi kuu.

 

Azam FC katika michezo miwili iliyocheza ya ligi hiyo, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, kisha wakashinda 2-0 dhidi ya Coastal Union, michezo yote ilifanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi jijini Dar.


Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya raundi mbili kukamilika inakwenda kumenyana na Mbeya City ya Mbeya ambayo ipo nafasi ya 18 baada ya kucheza mechi mbili pia.

 

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, amesema kuwa wao wanashukuru kuanza ligi vizuri kwa kupata pointi zote sita muhimu huku akisema kuwa kilichobaki kwao ni kuendeleza ushindi katika michezo inayofuata.

 

“Tunashukuru tumeanza ligi kwa ushindi katika michezo yetu miwili mfululizo, ni pointi sita muhimu kwetu ambazo tulikuwa tukizihitaji kutokana na malengo ambayo tumejiwekea msimu huu kuwa mabingwa wa ligi kuu.

 

“Kwa sasa baada ya ushindi huu ni kutafuta mwendelezo wa ushindi katika michezo yetu ijayo ili tujiwekee nafasi ya kuokota pointi nyingi mapema, hakuna kitu kinachoshindikana zaidi ya kujituma kwa wachezaji na kufuatisha maelekezo ya mwalimu,” amesema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *