Posted By Posted On

AZAM TV SASA KUONYESHA BUNDESLIGA LIVE MECHI ZOTE 360 KWA KIWANGO CHA HD

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KAMPUNI ya Azam Media Limited imetangaza rasmi kwamba msimu huu itaonyesha Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 18, mwaka huu.Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Azam Media Limited, Tabata TIOT Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Azam Media, Yahya Mohamed amesema kwamba wataonyesha Bundesliga kwa matangazo ya lugha ya Kiswahili kupitia kifurushi cha shilingi 18,000.“Tutaonesha Bundesliga katika kiwango cha HD kwa lugha ya Kiswahili kupitia kifurushi cha shilingi 18,000. “Mechi zote 360 tutazionyesha” amesema. Kwa upande wake mtangazaji nguli wa mpira, Charles Hillary ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha Redio cha UFM kinachomikiliwa na Azam Media pia alisema kwamba Watanzania watarajie burudani nzuri ya Bundesliga kwa sababu ni Ligi kubwa kihistoria. “Bundesliga ilianza mwaka 1963, Ujerumani ni taifa la wapenda kandanda, sisi kwa kuangalia hilo tumeamua kuwaletea burudani ya wapenda kandanda. Wachezaji wetu wa Tanzania wakiangalia hii, kuna mengi watajifunza” amesema Charles Hilary.,

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
KAMPUNI ya Azam Media Limited imetangaza rasmi kwamba msimu huu itaonyesha Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 18, mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Azam Media Limited, Tabata TIOT Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Azam Media, Yahya Mohamed amesema kwamba wataonyesha Bundesliga kwa matangazo ya lugha ya Kiswahili kupitia kifurushi cha shilingi 18,000.
“Tutaonesha Bundesliga katika kiwango cha HD kwa lugha ya Kiswahili kupitia kifurushi cha shilingi 18,000. “Mechi zote 360 tutazionyesha” amesema. 

Kwa upande wake mtangazaji nguli wa mpira, Charles Hillary ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha Redio cha UFM kinachomikiliwa na Azam Media pia alisema kwamba Watanzania watarajie burudani nzuri ya Bundesliga kwa sababu ni Ligi kubwa kihistoria. 
“Bundesliga ilianza mwaka 1963, Ujerumani ni taifa la wapenda kandanda, sisi kwa kuangalia hilo tumeamua kuwaletea burudani ya wapenda kandanda. Wachezaji wetu wa Tanzania wakiangalia hii, kuna mengi watajifunza” amesema Charles Hilary.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *