Posted By Posted On

BALE AINGIA ANGA ZA MANCHESTER UNITED

MANCHESTER United ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota wa Real Madrid, Gareth Bale ili ajiunge na kikosi hicho kinachonolewa na Ole Gunnar Solksjaer kwa msimu wa 2020/21.Solskjaer ana mpango wa wa kumvuta winga huyo ndani ya United ili kuongeza nguvu kwenye nafasi hiyo baada ya kupoteza matumaini ya kumpata nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho.Akiwa ndani ya Real Madrid tangu msimu wa 2013, Bale amecheza jumla ya mechi 171 na kupachika mabao 80 baada ya kuibukia ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki La Liga  akitokea Klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo inashiriki Ligi Kuu England.Bale ambaye kwa sasa yupo chini ya Kocha Mkuu, Zinedine Zidane anaweza kuondoka ndani ya timu hiyo inayotumia  Uwanja wa  Bernabeu ikiwa dili lake litakamilika kabla ya dirisha la usajili kufungwa Oktoba 5. ,MANCHESTER United ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota wa Real Madrid, Gareth Bale ili ajiunge na kikosi hicho kinachonolewa na Ole Gunnar Solksjaer kwa msimu wa 2020/21.

Solskjaer ana mpango wa wa kumvuta winga huyo ndani ya United ili kuongeza nguvu kwenye nafasi hiyo baada ya kupoteza matumaini ya kumpata nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho.

Akiwa ndani ya Real Madrid tangu msimu wa 2013, Bale amecheza jumla ya mechi 171 na kupachika mabao 80 baada ya kuibukia ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki La Liga  akitokea Klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo inashiriki Ligi Kuu England.

Bale ambaye kwa sasa yupo chini ya Kocha Mkuu, Zinedine Zidane anaweza kuondoka ndani ya timu hiyo inayotumia  Uwanja wa  Bernabeu ikiwa dili lake litakamilika kabla ya dirisha la usajili kufungwa Oktoba 5. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *